Bondia
Ibrahimu Class kushoto akipambana na Yohana Robart wakati wa mazoezi
yake ya kujiandaa na mpambnano wake na Simba Watundulu utakaofanyika
siku ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee.
Kocha
wa Mchezo wa ngumi Kambi ya Ilala Habibu Kinyogoli katikati
akiwaelekeza mabondia Yohana Robert KUSHOTO NA Ibrahimu Class jinsi ya
kutupa masumbwi kwa mpizani kwa kunyoosha mkono Class anajiandaa na
mpambano wake na Simba Watundulu siku ya Idi pili katika ukumbi wa
Diamond Jublee jijini Dar es salaam
Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu
KAMBI ya ngumi Ilala ipo kwenye maandalizi mazito ya kumnoa bondia Ibrahimu Class 'Ibra Mawe' anaetarajia kuzipiga na Simba Watundulu katika uzito wa KG,60 litakalofanyika siku ya Idi pili katika ukuimbi wa Diamond Jublee.
KAMBI ya ngumi Ilala ipo kwenye maandalizi mazito ya kumnoa bondia Ibrahimu Class 'Ibra Mawe' anaetarajia kuzipiga na Simba Watundulu katika uzito wa KG,60 litakalofanyika siku ya Idi pili katika ukuimbi wa Diamond Jublee.
Akizungumza
mmoja wa makocha wa kambi ya ilala inayongozwa na Kocha mkongwe
wa mchezo huo Habibu Kinyogoli, Rajabu Mhamila 'Super D', amesema
katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani wanamwandaa bondia
Ibrahimu Class kwa ajili ya mpambano huo utakaofanyika siku hiyo Super D
alisema wamemuandaa bondia wao kufanya vizuri ili kuweza
kumzibiti mpinzani wake kwa kuwa wanamjua uchezaji wake awapo ulingoni
hivyo wanamfundisha mbinu mpya kwa ajili ya kumkabili mpinzani wake.
Kambi
hiyo ya ngumi imewataka wadau wa mchezo uho kuja kuangali mchezo mzuri
wa masumbwi utakaonyeshwa na bondia wao kutoka kambi ya ilala Ibrahimu
Class anaetamba kwa jina la 'Ibra Mawe' ambaye yupo kwenye maandalizi
makali chini ya makocha wake Kinyogoli na Super D kwa ajili yampambano
huo na kuwataka wapinzani wake kwa sasa wakae chonjo kwa kuwa moto
umesha washwa na akuna wa kuuzima kwa bondia huyo chipkizi na mwenye nia ya kuupaisha mchezo wa masumbwi Kimataifa.
Mabondia
hao watakuwa wakicheza katika mpambano wa utangulizi wa RAUNDI 6 uku
pambano kuu ni kati ya Ramadhani Shauli wa Tanzania na Sande Kizito wa
Uganda watakaopambana kugombania mkanda wa Ubingwa wa IBF Afrika
No comments :
Post a Comment