Mkurugenzi wa Uhusiano na Masuala ya Sheria wa Kampuni ya Bia
(TBL), Bw. Stephen Kilindo (kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Simba,
Geofrey Nyange (kushoto) hundi ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya mkutano mkuu
wa klabu hiyo utakaofanyika tarehe 5 Agosti mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe na Katibu wa Simba, Evodius
Mtawala.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
25/7/2012
Ikiwa ni sehemu ya
udhamini wake kwa klabu ya Simba, bia ya Kilimanjaro Premium Lager leo
imekabidhi hundi ya Sh. Milioni 20 kwa klabu hiyo kwa ajili ya mkutano mkuu
utakaofanyika Agosti 5, mwaka huu jijini
Dar es Salaam.
Akikabidhi hundi
hiyo Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema: “Kilimanjaro Premium
Lager inatambua wajibu wake na ina nia ya dhati kuendeleza soka nchini. Kwa kwa
kuzingatia hilo
tungependa kuona maendeleo ya Simba na ndio maana tunaiunga mkono klabu hii
katika mkutano wake mkuu. Tunaamini kuwa mkutano huu utaimarisha uhusiano
uliopo kati ya klabu na wanachama wake kwa kuwapa fursa ya kuhakiki mwelekeo wa
klabu yao
waipendayo.Kavishe alieleza zaidi, “Mtu anapoangalia historia ya klabu hii
kongwe ambayo imejengeka kutokana na rekodi nzuri ya mafanikio kwa muda mrefu
utaona kwamba ina mamilioni ya wapenzi nchini. Soka ndio ndio mchezo mkubwa
zaidi hapa Tanzania
na bia ya Kilimanjaro imekuwa ikitoa mchango mkubwa kusaidia mchezo huu na ndio
maana leo tunasaidia mkutano mkuu wa Simba ili kusaidia kudumisha uwajibikaji
wa klabu kwa wanachama wake.
“Tunatambua wajibu
wetu kama wadhamini wakuu wa Yanga katika kutekeleza mkataba wetu, tutaendelea
kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha tunalipeleka soka la Tanzania kwenye
kilele cha mafanikio”.
No comments :
Post a Comment