Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, July 22, 2012

EDEN HAZARD AOTA KUWA LIONEL MESSI WA LIGI KUU ENGLAND




Eden Hazard
LONDON, England

“Messi ni Mchezaji Bora wa Dunia na nisenme wazi kwamba matarajio yangu ni kuwa mzuri kama yeye na naamini nitaweza”

YOSO mpya klabuni Staaamford Bridge, Eden Hazard, amepanga kufanya vitu vikubwa katika Ligi Kuu ya England na kusema atahakikisha anakuwa Lionel Messi wa ligi huyo pendwa duniani kwa sasa.

Mkali huyo mwenye miaka 21 raia wa Ubelgiji, ametua Darajani kwa dau nono la puani milioni 32 akitokea Lille ya Ufaransa na sasa anapania kujiweka juu sawa na thamani yake.

Nyota huyo hufurahi zaidi anapofananishwa na Messi Mchezaji Bora wa Dunia na shujaa wa FC Barcelona, ambapo alikataa ofa za kujiunga na klabu kubwa duniani ili kutimiza ndoto za kuchezea Blues.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kukamilisha uhamisho wake kutoka Ligue 1 na kutua Ligi Kuu, Hazard aliiambia SunSport: “Messi ni Mchezaji Bora wa Dunia na nisenme wazi kwamba matarajio yangu ni kuwa mzuri kama yeye na naamini naweza.

“Lakini nina furaha kubwa watu wanapofanya ulinganisho baina yetu na kunifananisha na Messi kunaniongezea ujasiri na kutafakari nia zitakazoniwezesha kupata mafanikio nikiwa Chelsea badala ya kuwaza vikwazo katika kunifikisha huko.

“Hatimaye kocha anabaki kuwa mtu wa mwisho kuamua kunichezesha mimi katika nafasi ambayo Messi anacheza akiwa Barca, lakini binafsi naangalia namna itakayonipa madfanikio kupitia njia nayopaswa kupitia.”

Mchezaji Bora Bora huyo wa zamani wa Ufaransa, alikataa ofa za kujiunga Manchester City na Manchester United kiangazi na kukubali dau la mshahara wa pauni 150,000 kwa wiki akiwa na jezi za Bluu za Chelsea, ambao ni mabingwa wa soka barani Ulaya.

No comments :

Post a Comment