Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, July 31, 2012

MABALOZI WA HARAMBEE YA UJENZI WA HOSTELI ZA WASICHANA WA SEKONDARI WAZINDUA KAMPENI YA ELIMU YAO WAJIBU WETU


Mabalozi wa kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA), Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog)  Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na asiyekuwepo ni Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004) ambaye alikuwa na udhulu na atakuwepo katika kampeni zinazoendelea.

Waandishi wa habari waliofika kuhudhuria uzinduzi wa ‘Elimu yao, Wajibu wetu” kampeni iliyoandaliwa na mabalozi waliojitolea kwa hiari kuhakikisha fedha hizo zinapatikana. Kiasi chote kitakachopatikana katika kampeni hiyo kitaingizwa katika mradi huu.


Kikundi cha wasichana maarufu watano katika nyanja mbalimbali nchini wameungana kwa pamoja na kuamua kwa hiari kuunga mkono jitihada za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) za kutafuta kiasi cha shilingi za kitanzania billion 2.3 zitakazotumika kujenga hosteli 30 ambazo zitahudumia wasichana wa shule za sekondari 1,504.

Kikundi hicho cha mabalozi wa kampeni hii kinaundwa na Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA) Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004), Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog) kiliguswa kwa namna ya kipekee na na jitihada za TEA na hivyo wakaamua kwa hiari kuungana na TEA katika kuhamasisha watu kujitokeza na kuchangia kampeni hii.

Mabalozi hawa wameiita kampeni yao “Elimu Yao. Wajibu wetu” maana ya usemi huu ni kwa kila mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha mtoto wa kike anapewa haki yake ya kuwa na elimu bora. Haki hii ya elimu inajumuisha mazingira mazuri ya kusomea. Hivyo huu ni wito kwa watanzania, wafanyabiashara, wafanyakazi, wanawake watanzania waliofanikiwa na watanzania wa ughaibuni kujitokeza kwa wingi na kuhusika moja kwa moja na jitihada hizi.

Changamoto ambazo mtoto wa kike anakumbana nazo hususani anayetokea nyumbani kwenda shule ni pamoja na kukosa muda wa kujisomea kutokana na kazi za nyumbani ambazo zinapelekea kuathiri maendeleo ya elimu kwa mtoto wa kike, mimba na ndoa za utotoni ni kati ya changamoto kubwa zinazowakumba wale waliopanga karibu na maeneo ya shule, kutokana na hayo, Mabalozi hawa wameamua kujitolea kwa kuweka mpango mkakati utakaosaidia ujenzi wa hosteli tano na kuendelea kati ya hizo 30 ambao TEA imepanga kujenga.

Mpango mkakati huo ni pamoja na kufanya kampeni katika vyomba mbalimbali vya habari nchini na kuandaa  mbio za hisani ambapo hela zitakazopatikana zitapelekwa katika mradi huo. Mabalozi hawa wanaamini kuwa tofali moja kutoka kwa kila mtanzania linaweza kuleta mabadiliko “changia Tofali”. Unaweza kuchangia kwa kutuma neno "Changia Tofali"kwenda namba 15564, na utakuwa umechangia Tshs 250/-. Changia mara nyingi uwezavyo.
Tunakuomba mchango wako wewe mzazi, wadau wa elimu na watanzania kwa ujumla wenu kuchangia katika kampeni hii. Mchango unaweza kuwa ni wa fedha taslimu au vifaa vya ujenzi wa hosteli na samani. Kwa upande wa fedha taslimu unaweza kuweka fedha katika akaunti ya “mfuko wa elimu” benki ya CRDB, namba ya akaunti 01J027639900 au kupitia akaunti ya M-pesa 404040, au tuma ujumbe Changia Tofali kwenda namba 15564. Pia unaweza kuleta mchango wako katika ofisi zetu zilizopo mikocheni barabara ya kambarage au kupitia vituo vya Televisheni vya ITV, Channel 10 na Star TV.

No comments :

Post a Comment