Msondo Ngoma
Twanga Pepeta
DAR ES SALAAM
BENDI
zenye ushindani mkubwa nchi za Twanga Pepeta na Msondo Ngoma
zinatarajiwa kupiga shoo ya aina yake kwenye tamasha la siku ya Wachaga,
(Chagga Day 2012), Julai 28, viwanja vya Leaders.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya
MyWay Entertainment, Paul Siboka walioandaa tamasha hilo, alisema siku
hiyo itakua ya aina yake kwa watu mbalimbali na familia zao
watakaojitokeza
Na kufurahia kwa pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki tamasha hilo.
“Siku
hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya utamaduni wa kabila
hilo la Chaga, na makabila mengine na burudani kutoka kwa bendi hizo za
Twanga na Msondo, pamoja na vikundi vingine vya ngoma ya asili ” alisema
Siboka.
Pia
alisema kua, kutakua na wazee wa mila ambo watazungumzia asili la
kabila la wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa
Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo,
ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha,
Siboka alisema baada ya Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia
tamasha lingine litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo
nbalo litapambwa na sherehe mbalimbali.
Siboka
pia aliwataja wadhamini wakuu wa tamasha hilo kua ni pamoja naTBL
kupitia bia za Safari na Kilimanjaro, SBC Tanzania (Pepsi), Dstv n
mengine mengi.
No comments :
Post a Comment