Arusha, Tanzania.
Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha kupitia hospitali yake ya AICC
kitaendesha kampeni ya kupima kisukari bure kwa wakazi wa Arusha ili
kusaidia wananchi kutambua kama wana ugonjwa wa kisukari au wapo katika
hatari ya kuugua ugonjwa huo.
Kampeni
hiyo itafanyika kesho (terehe 26-07-2012) katika hopitali ya AICC
iliyopo jijini Arusha ambapo madaktari wa hospitali ya AICC kwa
kushirikiana na madaktari wa wanaohudhuria mkutano wa Shirikisho la
Madaktari wa Kimataifa pamoja na madaktari kutoka Chama cha Ugonjwa wa
Kisukari Tanzania wataendesha zoezi la upimaji huo.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa AICC, Bwana Elishilia Kaaya, amesema kuwa mbali na
kupima kisukari, madaktari hao pia watatoa ushauri wa namna bora ya
kuishi na jinsi ya kuzuia madhara ya kisukari kwa wale watakao kuwa
wamekutwa na ugonjwa huo.
“Hospitali
ya AICC inatambua umuhimu wa afya za wakazi wa Arusha na Watanzania kwa
ujumla na ndio maana tumeona ni vema kufanya kampeni hii ya kupima
kisukari. Napenda kutumia fursa hii kuwaalika wakazi wote wa Arusha na
vitongoji nyake kufika kwa wingi kwani mbali na kupima pia itatolewa
elimu na ushauri kutoka kwa wataalamu hao.” alieleza Kaaya.
Kwa
mujibu Mkurugenzi Mwendeshaji, upimaji huo utaenda sambamba na mkutano
wa kwanza wa Shirikisho la Madaktari wa Kisukari wa Kimataifa ambao kwa
mara ya kwanza unafanyika hapa nchini. Mkutano huo utafanyika katika
kituo cha AICC ambapo madaktari wanaohudhuria mkutano huo na wale kutoka
Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania watatoa huduma ya upimaji katika
zoezi hilo.
“Tunaamini
baada ya kampeni hii wananchi watakuwa wamepata ufahamu juu ya hali ya
afya zao na kutumia vema ushauri wa madaktari kwa ajili ya kujikinga na
kuzua athari za ugonjwa huo”, alielezea Kaaya.
Mbali
na kuendesha kampeni hii, hospitali ya AICC imeanzisha kitengo maalumu
cha kisukari ambapo kila wiki madaktari hutoa huduma za matibabu na
ushauri kwa wagonjwa wa kisukri.
No comments :
Post a Comment