Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizindua mradi wa maji katika Hospitali ya Mawenzi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti anaemaliza
Muda wake wa, Richard Wells. Hadi kukamilika kwa mradi huo wa maji
safi, Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited imetumia zaidi ya
milioni 55 za kitanzania kujenga tanki kubwa la kuhifadhi maji kwa ajili
ya matumizi ya hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Teddy
Mapunda, akifafanua juu ya gharama halisi za mradi huo.
“Sisi
kampuni ya bia ya Serengeti tunatambua sana changamoto zinazowakabili
watanzania, taasisi na mashirika mbalimbali hususani hospitali juu ya
upatikanaji wa maji safi na salama, na kwasababu hiyo kampuni ya bia ya
Serengeti imeona hilo na kuamua kusadia kutatua tatizo hilo katika
maeneo mbalimbali ikianza katika maeneo yanayohitaji huduma ya maji kwa
haraka zaidi” alisema Mapunda na kuongeza kuwa kujitolea kusaidia jamii
ni moja yab sera za kampuni hiyo kama njia mojawapo ya kurudisha
shukrani zake kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.
Mgeni rasmi akifungua maji yanayotoka katika bomba lililounganishwa katika matanki hayo.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji wa SBL, Nandi Mwiyombela
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Mtumwa Mwako
Mkurugenzi
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Teddy
Mapunda, akifafanua juu ya gharama halisi za mradi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, anaemaliza muda wake Richard Wells akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
No comments :
Post a Comment