Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya
akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara ya waziri wa maji Prof.
Jumanne Maghembe mkoani humo. kushoto ni katibu tawala wa mkoa Alhaj
Salum Chima
NA
RAMADHANI JUMA,
AFISA
HABARI-SUMBAWANGA
MKUU
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya ameiomba serikali kuupatia kipaumbele
maalum mkoa huo katika miradi ya maji kutokana na kukabiliwa na upungufu wa
muda mrefu wa huduma hiyo.
Alitoa
ombi hilo kwa
waziri wa Maji Mh. Profesa Jumanne Maghembe wakati wa kikao cha majumuisho ya
ziara ya waziri huyo mkoa humo kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa
Mkoa.
Alisema
kuwa, licha ya tatizo hilo kuwa kubwa na la muda mrefu, huenda upungufu huo wa
huduma ya maji safi ukaongezeka mara dufu mara baada ya ujenzi wa barabara
zinazounganisha mkoa huo na ule wa Mbeya na Katavi kukamilika kwa kiwango cha lami,
hali itakayosababisha idadi ya watu kuongezeka kutoakana na shughuli za
kiuchumi kushamiri.
Manyanya
alipendekeza serikali kutekeleza miradi midogomidogo ya maji ya visima mkoani
humo ili kuwaharakishia wakazi wake huduma hiyo muhimu.
Kwa
upande wake, waziri Profesa Maghembe iliahidi kuwa, serikali itatekeleza miradi
ya maji katika vijiji 10 vya kila wilaya ya Mkoa huo ambazo ni Sumbawanga,
Kalambo na Nkasi.
Alisema
kuwa, utekelezaji wa mpango huo utaanza na vijiji vitatu katika kila wilaya na
tayari shilingi bilioni 1.4 zimetengwa kwa ajili awamu ya kwanza kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi ya maji katika miji ya Laela, Matai na kijiji cha
Nankanga.
No comments :
Post a Comment