Meli ya kisasa karibuni kuzinduliwa inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.
KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli
kubwa ya kisasa kwa ajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na
Unguja.
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15
mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa. Mohamedi
alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli
hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200
ambapo abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au
Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.
Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za
ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa
huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi
ya notkomail 20
No comments :
Post a Comment