Robin van Persie
LONDON, England
Dau
analotaka kama litakubaliwa na klabu yoyote litamfanya Van Persie kuwa
mmoja wa wachezaji wanalolipwa kiasi kikubwa zaidi duniani.
MHOLANZI Robin van Persie atahitaji dau la pauni milioni 10 kwa mwaka kwa klabu itakayohitaji kumsajili kiangazi.
Wakala wa
mshambuliaji na nahodha huyo wa Arsenal, Kees Vos alikuwa na kikao
kifupi na mabingwa wa soka nchini Italia Juventus na kufichua kuwa
nahodha huyo wa Washika Bunduki anahitaji mshahara wa pauni 195,000 kwa
wiki.
Dau analotaka
kama litakubaliwa na klabu yoyote litamfanya Van Persie kuwa mmoja wa
wachezaji wanalolipwa kiasi kikubwa zaidi duniani.
Awali Juventus
ilimtangaza RVP kama kipaumbele chao cha usajili wa majira ya joto,
kabla ya sasa kuonekana kurudi nyuma katika jaribio hilo linalohitaji
pesa kubwa, huku klabu hasimu za Manchester City na Manchester United
zikiwa tayari kupata saini ya nyota huyo mwenye miaka 28.
Mchezaji Bora
huyo mara mbili mfululizo, alishakataa kurefusha mkataba wake Emirates
kwa mshahara wa pauni 130,000, lakini sio Man City wala Man United
anayeweza kuiwa mgeni wa dau analohitaji nyota huyo kwa sasa.
Man City inamlipa
Yaya Toure mshahara wa pauni 225,000 kwa wiki, huku Wayne Rooney
akiigharimu Man United kiasi cha pauni 200,000 kwa wiki pia.
Kocha wa Arsenal,
Arsene Wenger amemuacha RVP katika ziara ya kikosi chake kujiandaa na
msimu mpya huko Mashariki ya Mbali na kuna fununu kwamba Lukas Podolski
anatarajiwa kukabidhiwa rasmi jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na Van
Persie.
Na Wenger ambaye
tayari keshawasajili washambuliaji wawili, Podolski na Olivier Giroud,
huku akimfukuzia Fernando Llorente, amekiri kuwa RVP ni muhimu: “Van
Persie ni mmoja wa washambuliaji bora duniani.”
No comments :
Post a Comment