Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, March 25, 2010

SIMBA YAPATWA NA KIGUGUMIZI UJIO WA PHIRI

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Wekundu wa Msimbazi Simba wameanza maandalizi kwaajili ya mchezo wao wa marudiano wa kombe la Shirikisho dhidi ya Lengthens ya Zimbabwe utakaopigwa Jumapili April 4 kwenye uwanja wa UHURU Dar Es Salaam huku kocha wa kikosi hicho Mzambia Patrick Phiri akishindwa kuwasili hapo jana kama alivyotakiwa.

Akizungumza kutoka nyumbani kwao Zambia Phiri amesema kuna masuala yamemkwamisha na pale atakapoyakamilisha ndipo atarejea nchini.

Phiri alipoulizwa lini hasa atarejea kati ya kesho Ijumaa au Jumamosi akasema atabainisha pale atakapokuwa na uhakika lakini akisema huenda kambi ya kikosi hicho ikawekwa Zanzibar kuanzia Jumatatu huku akisema hata kama angewahi kurudi programme yake isingetimia kwakuwa kuna wachezaji takribani nane wapo kwenye kikosi cha Taifa Starz kinachocheza na SOMALIA .


Wekundu hao tayari wameanza maandalizi yao bila ya Phiri wakiwa chini ya kocha msaidizi Amri Said wakianza na mazoezi ya ufukweni.

WAPINZANI WA TAIFA STARS - SOMALIA WAWASILI


Timu ya Taifa ya Somalia The Ocean Starz imetua leo tayari kwa mchezo wake wa Jumamosi dhidi ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Starz kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa bingwa barani Africa CHAN utakaopigwa kwenye uwanja wa UHURU.

The Ocean Starz imetua ikiwa na msafara wa watu 25 huku ikiwa na matumaini makubwa ya kuishinda Starz hapo Jumamosi.

Nahodha wa kikosi hicho Yusuph Ali Nur amesema mchezo huo utakuwa mgumu lakini wamejiandaa vyema kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Msafara uliowasili leo ni pamoja na viongozi Abdikani Said Arab,Basher Mohamed Gesey,Yaxye Maxamed Abukar,Mohamed Abdulle Farayare na Abdulkadir Abdirahman Ali.

Wachezaji ni pamoja na Dahir Mohamud Mukhtar,Wa’di Kassim Hassan,Mohamed Abdullahi Aboki,Osman Yusuf Osman,Tahlil Mohamed Mohamud,Hassan ahmed Mohamed,Hassan Ali Roble na Kamal Ali Omar.

Wengine ni Nahodha Yusuf Ali Nur,Mohamed Hashi Siyad,Mohamed Hassan Ali,Abdifitah Abdi Osman,Badri Moallin Ahmed na Jabril Hassan Mohamed.

Ndani ya kikosi hicho pia wamo Mahad Mohamed Haji,Aadan Hussein Ibrahim,Mustaf Hassan Mohamed,Anwar Sadad Ibrahim,Sidi Said Abdulla na Mohamed Yare Isak.

Wakati huo huo Benki ya NMB leo wamekabidhi kiasi cha shilingi milioni 21 kwa Taifa Starz ikiwa ni maandalizi kwa mchezo huo wa Jumamosi dhidi ya Somalia The Ocean Starz.

Mbali na fedha hizo Starz imekabidhiwa vifaa mbalimbali vya michezo vikiwemo jezi,vizuia ugoko(Shin Guard),viatu,soksi na bips vyote vikiwa na thamani ya kiasi cha shilingi milioni 15.

Mkuu wa Masoko wa benki ya NMB IMANI KAJULA amesema wametoa vifaa hivyo kutambua umuhimu wa mchezo huo wa Jumamosi.


Naye Katibu Mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF FREDRICK MWAKALEBELA amesema maandalizi kiutawala tayari yamekamilika na vifaa hivyo vitasaidia pia kwa mchezo dhidi ya Rwanda Amavubi kama watafanikiwa kuwaondoa The Ocean Starz Somalia.

Wednesday, March 24, 2010

FRANK RIBERY SIWEZI KUIMBA WIMBO WA CHELSEA

Mchezaji FRANCK RIBERY ametupilia mbali madai ya kujiunga na klabu ya Chelsea kipindi cha majira ya joto.

Ribery, mwenye umri wa maika 26, anamkataba na klabu yake ya Bayern Munich hadi mwaka 2011 na klabu hiyo kongwe nchini Ujerumani bado inataka kumuongezea mkataba.

Chelsea haijafanya siri kuhusu nia yao ya kkutaka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa lakini inaonekana suala la kutua Stamford Bridge kuwa gumu kuliko kwenda nchini Hispania.

Amesema licha ya Klabu ya Chelsea kuwa ni klabu kubwa, lakini ni bora nikaenda kucheza soka nchini Hispania endapo nitaamua kuondoka Bayern.

BAFANA BAFANA YATARAJI KUCHEZA MICHEZO MIWILI YA KIRAFIKI BRAZILI

kocha wa Bafana Bafana Carlos Alberto Pereira
Vyombo vya habari vya Brazili vimeripoti kuwa kocha Carlos Alberto Parreira amethibitisha kwamba Bafana Bafana itacheza michezo miwli ya kirafiki na klabu za juu nchini Brazili ikiwa ni pamoja za Sao Paulo, Palmeiras na Santos, kabla ya kurejea nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo, imeongezwa kuwa michezo yote hiyo miwili Bafana Bafana itatumia wachezaji wake wa akiba.

Siku ya Jumatatu, Raisi wa klabu ya Palmeiras FC nchini Brazilil, Luiz Gonzaga Belluzzo, alisema hana taarifa ya uewpo wa mchezo dhidi ya Bafana Bafana ambao umepangwa kuchezwa siku ya Jumamosi kufuatia uwanja wao kutumiwa na klabu za ligi daraja la nne, klabu za Verdao na Mirassol, wakati mratibu wa michezo wa klabu hiyo Antonio Biasetto, naye akiungeza kusema kwamba hana taarifa mipango ya mchezo huo.

FIFA YAIONGEZEA TANZANIA TIKETI 90 ZA KOMBE LA DUNIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
24/03/2010

FIFA YATOA TIKETI ZA NYONGEZA ZA KOMBE LA DUNIA 2010

TFF inapenda kuutaarifu umma wa watanzania hususan wapenzi wa mpira walioomba kununua tiketi za Kombe la Dunia kuwa shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu, FIFA limekubali maombi ya TFF ya tiketi za nyongeza.Itakumbukwa kuwa maombi ya tiketi yalikuwa mengi kuliko idadi ya tiketi 290 ambazo Tanzania ilikuwa imetengewa na FIFA. Maombi yaliyozidi yalikuwa 450 kwa michezo tafauti. Hata hivyo maombi mengi zaidi yalikuwa katika michezo ya robo fainali, nusu fainali na fainali.

Kwa sasa tiketi za nyongeza ambazo FIFA imeipatia Tanzania ni 90 (tisini)

Tiketi zote hizo ni za mchezo namba 61 ambao ni wa nusu fainali ya kwanza itakayochezwa Cape Town kwenye uwanja wa Green Point Julai 6 2010.

Tiketi ya bei chini ni Dola za Marekani 250 na ya bei ya juu ni dola 600.

Watakaopewa kipaumbele cha kununua tiketi hizi za nyongeza ni wale ambao waliomba lakini hawakuwafanikiwa kupata tiketi katika mgawo wa awali.Baada ya hapo watafikiriwa waombaji wengine ambao watakuwa tayari kulipa.

Hivyo basi wale wote waliowasilisha maombi wanatakiwa kufika ofisi za TFF kwa ajili ya kulipia tiketi zao.

Ifahamike kuwa kama ilivyokuwa kwa tiketi zilizouzwa awali kutakuwepo ada ya asilimia kumi (10) kwa kila tiketi kwa ajili ya utawala na gharama za kutuma fedha FIFA. Malipo yote ni tasilimu katika dola za Marekani.

Mwisho wa kulipia tiketi hizi ni April 2, 2010.


Fredrick Mwakalebela
KATIBU MKUU

Tuesday, March 23, 2010

FIFA KUSIKILIZA KESI YA SHAMBULIO LA ALGERIA MISRI

Shirikisho la kandanda Duniani FIFA inatarajiwa kusikiliza madai ya shambulio lililofanywa nchin Misri wakati Algeria kabla ya mchezo wao wa kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia mjini Cairo tarehe 15 April.FIFA imesema kwamba kamati ya nidhamu itasikiliza kesi hiyo watakapokutana Zurich.
kwa mujibu wa sheria za kinidhamu za FIFA zinaitaka nchi mwenyeji kuhakikisha usalama wa wageni.
Chama cha soka cha Misri kinaweza kutozwa fainali, ama wanaweza kupewa adhabu ya kutochezewa michezo ya kimataifa nchini mwao.wachezaji wa Algeria na viongozi wao walijeruhiwa na vioo vilivyopasuliwa kwa kushambuliwa na mawe na mashabiki wa Misri kabla ya mchezo mwaka jana mwezi Novemba.
Misri ilishinda mchezo huo kwa magoli 2-0 na kulazimisha kuchezwa mchezo wa mtoano nchini Sudan, ambapo Algeria ilishinda 1-0 na kufanikiwa kutinga fainali za kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.

TFF - SIMBA, TAIFA STARS NA TWIGA STARS WAWAKILISHA KIMATAIFA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TIMU YA TAIFA - TWIGA STARS
Twiga Stars imefaulu kusonga mbele katika mashindano ya kuwania kufuzu kwa fainali za saba za Afrika kwa wanawake zitakazofanyika Afrika Kusini baadaye mwaka huu baada ya kuitoa Ethiopia kwa ushindi wa jumla ya magoli 4-2.
Ni dhahiri kuwa ushindi huo umetokana na kujituma kwa wachezaji, mbinu sahihi za mwalimu na wasaidizi wake wa jopo la ufundi pamoja na matunzo ambayo timu hiyo ilipewa wakati wakijiandaa na mchezo huo na jamii kwa jumla.
Twiga Stars bado inakabiliwa na michezo miwili dhidi ya Eritrea ambapo mchezo wa kwanza utafanyika hapa nyumbani tarehe 22 Mei 2010 na mchezo wa marudiano utafanyika majuma mawili baadaye huko Asmara.
TFF inafahamu umuhimu na ina nia thabitri ya kuandaa timukikamilifu pale inapokabiliwa na mashindano.
Timu zote za Taifa zimekuwa zikitayarishwa katika mazingira ya kuridhisha kulingana na hali halisi iliyopo.
Katika hali hhii Twiga Stars, kama ilivyo kwa timu nyingine zisikuwa na udhamini wa kimkataba itaendelea kuandaliwa vizuri kulingana na hali halisi.Tunapenda pia kwa mara nyingine kuomba makampuni ya kibiashara, taasisi mbali mbali, serikali na jamii kwa jumla kuisaidia timu hii ili iweze kuliwakilisha vema taifa.
TFF tayari imeanza mazungumzo na makampuni kadhaa juu ya utekelezwaji wa programu ya mwalimu Charles Boniface Mkwasa.

2. USHIRIKI WA TIMU YA SIMBA KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA

Timu ya Simba imefanikiwa kupata ushindi mkubwa wa magoli 3-0 ugenini dhidi ya timu ya Lengthens ya Zimbabwe katika kombe la shirikisho.
TFF inapenda kuwapongeza Simba ambao ni wawakilishi pekee wa nchi waliosalia katika michuano ya kimataifa.
Tunafahamu fika kuwa bado kuna mchezo wa marudiano utakaofanyika kati ya tarehe 3 na 4 April 2010, ambao Simba wanahitaji kufanya vema ili kuendelea kulinda heshima ya nchi.
TFF inapenda kuwahakikishia simba kuwa itashirikiana kwa kila hali na simba ili kuhakikisha wanafanya vema kwenye mchezo huo na mingine itakayofuata.

3. TIKETI ZA KOMBE ;A DUNIA 2010.
Kama tulivyotangaza awali FIFA iliitengea Tanzania tiketi 290 Kombe la Dunia litakalofanyika Afrika Kusini Juni hadi Julai 11, 2010.
Ladhalika tilitangaza kuwa watu wote walikuwa wameomba kununua tiketi hizo wazilipe ili kwa fedha ziwasilishwe FIFA na hatimaye tiketi zitumwe nchini.
Tunapenda kuutangaza umma kuwa tumefanikiwa kuuza tiketi zote 290 ambazo FIFA iliitengea Tanzania.
Tiketi zilizouzwa zinathamani ya Dola za Marekani 62,710. Fedha hizo tayari zimetumwa FIFA ili waweze kuleta zilizonunuliwa.
TFF inawashukuru wote waliolipia tiketi zao walizoomba.
Tumewaandikia tena FIFA kuwaeleza na kuwakumbusha kuwa maombi tuliyokuwa nayo yalikuwa mengi kuliko mgawo wa tiketi walizotupatia hivyo watufikirie katika tiketi za nyongeza tulizoomba. Matarajio ni kwamba watatufikiria kjwa kuzingatia idadi ya tiketi zilizonunuliwa kwenye mgawo.

4 TIMU YA TAIFA - TAIFA STARS

Taifa Stars inahceza na timu ya Taifa ya Somalia Jumamosi hii Machi 27, 2010 katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani zitakazofanyika Sudan Januari 2011.
Taifa Stars inaendelea na kambi yake chini ya mwalimu Marcio Maximo na mazoezi yanakwenda vizuri tayari kwa kuwakabili wa Simalia.
Mchezo dhidi ya Somalia unachezwa mmoja tu kwa vile Somalia iliiomba Tanzania na CAF kutokana na Shirikisho la Mpira wa miguu la Somalia kutokuwa na uwezo wa kuandaa mchezo wa nyumbai huko Djibout, ifahamike kuwa Somalia kwenyewe hakuna mazingira ya kucheza mashindano ya kimataifa.
Kwa hiyo mchezo huo wa Jumamosi lazima utoe mshindi na kama mshindi hatakuwa amepatikana baada ya dakika tisini (90) itabidi itumike changamoto ya mikwaju ya penati kumpata mshindi.
Mshindi atacheza na Rwanda. Iwapo Taifa Stars itafaulu kusonga mbele itaanza nyumbani dhidi ya Rwanda hapo Mei Mosi badala ya Mei 22. Hii ni kufuatia CECAFA kuiomba CAF Kurejesha nyuma michezo ya kufuzu kwa CHAN kwa ukanda huu ili kutoa fursa ya kuchezwa kwa kombe la Kagame kuanzia Mei 15 - 29.
Kwa sasa yanangonjewa mawasiliano ya CAF.
Mchezo wa Somalia utafanyika uwanja wa Uhuru kuanzia saa tisa 9 Alasiri.

Viingilio

Viingilio vimewekwa katika makundi manne kama ifuatavyo:

VIP (RANGI YA BLUU) - 30,000/=
Jukwaa kuu - Nyekundu & Njano - 15,000/=
Jukwa la kijani - 10,000/=
Mzunguko - 3,000/=

Waamuzi

Waamuzi wanatokea Kenya, Mwamuzi wa kati ni Kirwa Sylvester, msaidizi wa kwanza ni John Ngururi, msaidizi wa pili ni Range Marwa Aden wakati msaidizi wa akiba Israel Mujuni Nkongo wa Tanzania. Kamishna ni Hussein Fadoul wa Djibout.
Timu ya Somalia inatarajiwa kuwasili Alhamisi saa saba mchana kwa ndege ya shirika la ndege la Ethiopia na itakuwa na msafara wa watu 25.
TFF inawaomba watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi kuiunga mkono mkono timu ya taifa ili iweze kufanya vema katika harakati za kufuzu kwa mara ya pili mfululizo.
Kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN).

Fredrick mwakalebela.
KATIBU MKUU - TFF

Monday, March 22, 2010

SERIKALI NGUMI TUNATAKA VIFAA

Serikali imeombwa kusaidia vifaa vya mazoezi ya mchezo wa ngumi za ridhaa ili timu taifa ijiandae vizuri katika michuano ya jumuia ya madola itakayoanza Oktoba mwaka huu New Delh nchini India.

Akizungumza na kipindi hiki Naodha wa timu ya taifa ya mchezo wa ngumi Joseph Martini amesema wametembelea nchi mbalimbali na kuona mabondia wenzao wanavyofanaya mazoezi na vifaa vizuri lakini kwa upande wao wanashindwa kufanya mazoezi vizuri kutokana na tatizo la vifaa.

RIADHA TANZANIA KUONDOKA MACHI 25 KWENDA POLAND

Timu ya taifa ya mchezo wa riadha inatarajia kuondoka nchini marchi 25 kuelekea nchini Poland kushiriki mashindano ya Dunia ya Mbio za nyika yatakayoanza marchi 28 mwaka huu nchini humo.

Maashindano hayo ya kila mwaka yanashirikisha wachezaji wote kutoka nchi zote zinashiriki mchezo huo huku timu ya Tanzania ikiwakilishwa na wachezaji kumi na moja.

Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania AT, Suleimani Mujaya Nyambui amesema kwamba kwa sasa wapo katika maandalizi ya mwisho mwisho ili kuhakikisha timu inaondoka bila ya matatizo yeyote.

Sunday, March 21, 2010

AMINA KINARA WA GOFU LUGALO INAYODHAMINIWA NA ZAIN


Mchezaji wa gofu Amina Khamis akijiandaa akipiga mpira wakati wakati wa mashindano ya gofu yaliyofanyika katika viwanja vya gofu vya Lugalo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Amina aliibuka mshindi wa jumla katika mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na kampuni ya Zain.

Amina Khamis meibuka mshindi wa jumla katika mashindano ya gofu yaliyofanyika katika viwanja vya mchezo huo vya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kupata jumla ya pointi 23.

Mashindano hayo ambayo yanafanyika kila mwisho wa wiki chini ya udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania yalishirikisha wachezaji katika makundi manne, akina mama, wasichana,vijana wa kiume na wazee.

Kufuatia ushindi huo Amina alijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo kifurushi cha Zain ambacho kina fulana, begi na vifaa vingine vya michezo kutoka Kampuni ya Simu za mkononi ya Zain ambao ndiyo wadhamini wakuu wa mashindano hayo.

Akiongea baada ya kukabidhiwa zawadi zake Amina mbaye ni mchezaji chipukizi ambaye kwa sasa ni kati ya wachezaji wanaoonyesha viwango vya juu katika gofu katika klabu ya Lugalo, alisema kuwa kwa sasa matumaini yake ni kucheza kufikia katika kiwango cha kimataifa.

Alisema kuwa kinachomtia moyo yeye na vijana wenzake ni jitihada za kampuni ya Zain katika kudhamini mchezo wa gofu katika klabu ya Lugalo, hali ambayo imesaidia kuinua viwango vya gofu kwa vijana wa klabu hiyo.

Washindi wengine ni Gidion Sayore na Rapahel Letara kwa upande wa wazee,Abdala Idd kwa vijana wa kiume na Stepania Sayore kwa wanawake.Mchezaji gofu Sophia Mathiasi akipokea zawadi kutoka Zain baada ya kuibuka mshindi wa pili katika mashindano ya gofu yaliyofanyika juzi kwenye viwanja vya gofu vya Lugalo.

TWIGA STARS HUREEEEE....YATINGA HATUA YA PILI MATAIFA YA AFRIKA (WANAWAKE)

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Wanawake 'Twiga Stars' Esther Chabruma (kulia) akikabiliana na mabeki wa Ethiopia, Semira Kemar Aman na Beziihan Endale Alemar wakati wa mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika uliofanyika kwenye Uwanja wa wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Timu ya taiafa ya wanawake Tanzania Twiga Stars imefanikiwa kutinga hatua ya pili ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa wanawake baada ya kutoka sare ya kufungana goli 1-1 katika mchezo wa marudiano uliyochezwa Jumamosi uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Twiga Stars inasonga mbele kwa jumla ya magoli 4-2 baada ya mchezo wa kwanza kushinda 3-1 walipokutana nchini Ethiopia majuma mawili yaliyopita.

Katika mchezo wa jana timu ya Twiga Stars licha ya kufanikiwa kusonga mbele lakini ilionekana kucheza mpira katika kiwango cha chini tofauti na Ethiopia ambao walikuwa wakionekana kucheza mpira wenye mipango ya kusaka ushindi.

Sasa Twiga Stars itakutana na Eritrea katika hatua ya pili ya kusaka nafasi ya kucheza mataifa ya Afrika soka la wanawake, fainali ambazo zitafanyika nchini Afrika Kusini mwaka huu.

Saturday, March 20, 2010

SIMBA WAREJEA TANZANIA KISHUJAA

Wachezaji wa Simba wakilakiwa na mashabiki waliyojitokeza kuwapokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, mwenye begi wa kwanza ni Mohammed Banka ambaye alifunga goli la pili, na wanyuma ni Juma Jabu "JJ".

MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba walimchelewesha Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere baada ya kutaka kuwashuhudia mashujaa hao.

Simba walirejea wakitokea Zimbabwe katika mchezo wao wa Kombe la CAF dhidi ya Lengthens FC ambapo walishinda mabao 3-0 yaliyofungwa na Mussa Hassan Mgosi, Mohamed Banka na Mohamed Kijuso.
Kundi la Friends Of Simba likiwapungia mashabiki wa Simba ambao walijitokeza kuwalaki wakati wakirejea toka nchini Zimbabwe, Mwenye kanzu ni Kassim Dewji.
Mabingwa hao walipata mapokezi ya nguvu kutoka kwa wapenzi wa timu hiyo japokuwa waliwasiri majira ya saa 3 asubuhi kwa ndege ya shirika la Kenya.

Makamba ambaye alikuwa na shughuli zake uwanjani hapo lakini alipowakuta mashujaa hao wakishuka alisimama na kuanza kusalimiana na wachezaji na kuwaahidi kuwapa chakula cha mchana.
Golikipa Juma Kaseja akisalimiana na mashabiki wakati wakiwasili mapema leo toka nchini Zimbabwe.
Akizungumzia mchezo huo, Kipa wa Simba, Juma Kaseja alisema mchezo ulikuwa mgumu sana lakini kutokana na maandalizi waliyofanya ilikuwa chachu ya ushindi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa klabu hiyo, Hassan Dalali alisema timu yake hawatabweteka na ushindi waliopata kwani wapinzani wao si wa kubeza.

Dalali ambaye alikuwa mkuu wa msafara wa Harare alisema watajipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi mnono katika mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili zijazo.

KAMPUNI YA BUSINESS TIMES "THE BIZE" MABINGWA KOMBE LA NSSF

TIMU ya soka ya Kampuni ya Business Times, 'The Bize' imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa michuano ya NSSF Media Cup 2010, baada ya kuichapa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo ya Zanzibar kwa penalti 9-8, katika fainali zilizofanyika katika uwanja wa TCC Chang'ombe, Dar es Salaam.
Ubingwa huo ni zaidi ya ubingwa wa Simba kwani The Bize imetwaa ubingwa huo bila ya kupoteza mchezo hata kutoa sare wakati mabingwa wapya wa Bara wametoka sare michezo miwili.
The Bize hadi wanatinga hatua ya fainali na kutwaa ubingwa huo, waliichapa Radio Kheri mabao 2-0. kabla ya kuitandika NSSF mabao 2-1 na kuishushia kiama IPP mabao 6-0.
Kwa ushindi huo The Bize walijinyakuliwa kitita cha sh. milioni 3 na kikombe walichokabidhiwa na Waziri wa Michezo na Utamaduni George Mkuchika ambaye alikuwa mgeni rasmi katika fainali hiyo.
The Bize waliwainua mashabiki wao dakika ya 17 ya mchezo huo kupitia kwa Martin Peter baada ya kuachia shuti kali akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Dismas Bahatia.
Wakitandaza kandanda safi huku wakigongeana pasi fupi fupi, The Bize waizidisha mashambulizi langoni mwa wapinzani wao ambapo dakika ya 43 walipata bao la pili lililofungwa na George Dennis kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Habari Zanzibar Abduhim Juma.
Kipindi cha pili Zanzibar walicharuka na kuanza kulisakama lango la The Bize na dakika ya 60 walipata bao la kwanza lililofungwa na Abduhim Juma kwa njia ya penalti baada ya mabeki kucheza rafu katika eneo la hatari.
Habari Zanzibar walisawazisha bao la pili katika dakika ya 75 kupitia kwa Amour Mussa baada ya mabeki wa The Bize kujichanganya.
Kufuatia matokeo hayo mpaka mwisho wa mchezo zilipigwa penalti ambapo The Bize ambao pia ni wachapishaji wa magazeti ya Majira, Spoti Starehe, Business Times na Dar Leo waliibuka na ubingwa baada ya kuichapa Habari Zanzibar kwa penalti 9-8.
Katika mchezo wa soka The Bize walizawadiwa kombe pamoja na kitita cha sh. milioni 3, wakati nafasi ya pili ilichukuliwa na Habari Zanzibar ambao walipewa kombe na sh. milioni 2 na Mwananchi waliambulia milioni 1.
Katika mchezo wa Netiboli NSSF walishika nafasi ya kwanza baada ya kuichapa Mwananchi kwa mabao 44-12 na walizawadiwa kombe na sh. milioni 2.5, Mwananchi Queens walipata sh. milioni 1.5 wakati The Bize Queens waliambulia sh. 750,000 na wafungaji bora wa netiboli ni Lulu Habibu wa The Bize Queens ambaye ana mabao 65 wakati mfungaji bora kwa upande wa soka ni Majuto Omary wa Mwananchi na wote walipata sh. 200,000 kila mmoja.

Friday, March 19, 2010

SIMBA YAISASAMBUA LENGTHEN FC, ZIMBABWE

Klabu ya Simba imefanikikwa kuanza vema michuano ya kombe la shirikisho nchini Zimbabwe dhidi ya klabu ya Lengthen FC kwa kuichapa goli 3-0.
Mashuja wa simba katika mchezo wa leo walikuwa n Mohammed Banka aliyefunga goli la kwanza na Musa Hassan "Mgosi" aliyefunga goli la pili katika kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili ambacho kilianza kwa kasi huku klabu ya Lengthen Fc ikifanya jitihada za kusaka hata goli moja la kufutia machozi lakini walinzi wa Simba walifanya kazi nzuri ya kuwadhibiti safu ya washabuliaji wa klabu hiyo changa ya Zimbabwe.
MOhammed Kijuso ndiye aliyehitimisha karamu ya magoli 3-0 kwa Simba.
Ushindi huo unaifanya Simba sasa kutengeneza mazingira mazuri ya kusonga mbele, pindi watakapokutana wikki mbili zijazo katika mchezo wa marudiano ambapo Simba sasa itakuwa nyumbani.
Klabu ya Simba inatarajiwa kureje Tanzania Kesho asubuhi kuanza maandalizi ya mchezo wa marudiano.

TFF YAONGEA DHIDI YA KUKAMATWA KWA TIKETI BANDIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
19/03/2010

Jumatatu tarehe 15/03/2010 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Moro United uliofanyika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, mmoja wa wauza tiketi, Mohamed Baruani alikutwa na kitabu kimoja cha tiketi ambacho hakikuwa miongoni mwa vitabu vilivyokabidhiwa rasmi kwa wauzaji wa tiketi.Wakati akihojiwa muuzaji huyo alisema alikabidhiwa kitabu hicho cha tiketi na mmoja wa maofisa wa TFF wanaohusika na masuala ya tiketi.
Kutokana na hali hiyo maofisa wa Polisi waliendelea kufuatilia ikiwemo kuwahoji wahusika.
Miongoni mwa hao waliohojiwa na kwa maana hiyo wanalisaidia jeshi la polisi, ni afisa wa TFF Daniel Msangi pamoja na baadhi ya watendaji wa kiwanda cha Inter Press of Tanzania Limited, ambao ni wachapishaji wa tiketi za mchezo kati ya Yanga na Moro United.
Kwa mantiki hiyo suala hili lipo mikononi mwa Polisi na linashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za kisheria.
TFF inashukuru na kuwapongeza wale wote waliotoa taarifa ambazo baadaye zilifanikisha kubainika uwepo wa kitabu kilicho nje ya utaratibu na inaahidi kwa dhati kuwa itatoa kila aina ya ushirikiano kwa jeshi la Polisi katika kushughulikia jambo hili.
Kwa kuwa tukio hili bado limo mikononi mwa Polisi na linafanyiwa kazi kwa utaratibu wa kisheria ni vema TFF, wadau wa mpira na jamii kwa jumla kuwa na subira na kuicha dola kufanya kazi yake.
TFF inachukia vitendo vyovyote vinavyosababisha kuvuja kwa mapato yatokanayo na viingilio vya mpira wa miguu na inayo nia ya dhati ya kuhakikisha fedha zinazopatikana kwenye mpira zinausaidia mpira wenyewe.
Katika kutekeleza hilo TFF iliunda Kamati maalumu ambayo pamoja na mambo mengine ni kazi yake ni kukusanya maoni ya wadau ili kubaini na hatimaye kuziba mianya ya upotevu wa fedha zitokanazo na mapato ya viingilio.

Fredrick Mwakalebela
KATIBU MKUU

TWIGA STARS JUMAMOSI KUIVAA ETHIOPIA

Timu ya taifa ya Tanzania ya wanawake Twiga Stars Jumamosi itashuka dimbani kuikabili timu ya taifa ya Ethipia ya wanawake katika mchezo wa kuwani kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika zitakazochezwa huko nchini Afrika kusini baadae mwaka huu.
Twiga stars hiyo kesho wanashuka katika dimba la Uhuru jijini Dar es salaam huku wakichagizwa na kumbu kumbu ya ushindi wa mabao matatu kwa moja walioupata dhidi ya wapinzani wao katika mchezo wa kwanza uliounguruma majuma yaliyopita huko mjini Adis Ababa nchini Ethiopia.
Akiuzungumzia mchezo huo wa Jumamosi raisi wa chama cha soka la wanawake nchini Lina Madina Muhando amesema mchezo huo utakua mgumu kwa pande zote mbili lakini shilingi ya ushindi akaiangushia kwa Twiga Stars.
Lina Madina Muhando pia amewataka watanzia kwa ujumla hususana kina mama kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa uhuru hapo kesho.
Katika kuhakikisha wimbi la ushindi linaendelezwa katika mchezo huo wa Jumamosi kampuni ya bia ya Serengeti imetoa msaada wa shilingi milion 4.5 kama msaada ambao umekua ukihitajika kwa hali na mali katika timu hiyo ya wanawake.
Msaada huo wa kampuni ya bia ya Serengeti umewasilishwa TFF hii leo na Afisa Uhusina na mawasiliano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda ambae pia amewataka watanzani kujitokeza uwanjani kwa wingi hiyo kesho kuishangilia Twiga Stars.
Nayo kampuni ya CXC HOLDING kupitia kwa mkurugenzi wake Charles Hamka nayo imekabidhi hundi ya shilingi milion kumi kwa lengo la kuisaidia timu hiyo.
Wakati misaada hiyo ikitolewa kwa lengo la kuisaidia timu ya Twiga Stars, kocha mkuu wa timu hiyo Charles Boniphas Mkwasa amesema kikosi chake kitaingia uwanjani kwa lengo la kuendeleza mazuri waliyokwisha yaanza huko nchini Ethiopia majuma mawili yaliyopita.
Kwa upande wake nahodha wa Twiga Stas Sophia Mwasikili nae amewaahidi ushindi watanzani kwa ujumla huku akiweka bayana malengo yao mwaka huu ni kucheza fainali za mataifa ya Afrika huko nchini Afrika kusini.

TMK WADAI KUHUJIMIWA LIGI DARAJA LA KWANZA

Baada ya kubanjuliwa mabao matatu kwa moja kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora dhidi ya AFC, mmiliki wa timu ya TMK UTD Abass Mtemvu ameonyesha kuchukizwa na sababu zilizopelekea kufungwa kwa timu hiyo.
Mtemvu amelazimika kuzungumzia sababu hizo hii leo alipokutana na waandishi wa habari, kufuatia kuibuka kwa toka kwa mashabiki walioushuhudia mchezo huo ambao wamedai wenyeji AFC walipata ushindi katika hali ya ndivyo sivyo.
Amesema pamoja na hatua hiyo ya AFC kupata ushindi wa ndivyo sivyo pia viongozi wa timu ya TMK Utd walipigwa na askari jeshi waliokua wakilinda usalama kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Michuano hiyo imeendelea tena hii leo katika uwanja wa sheikh mari Abaeid kwa kuchezwa michezo miwili ambapo katika mchezo wa kwanza timu ya Rhino toka mkoani Morogoro ilicheza na Polisi Dodoma.
Matokeo ya mchezo huo ni kwamba maafande wa jeshi la p[olisi toka mkoani Dodoma wamefanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.
Mchezo wa pili ulikuw akati ya timu ya Ruvu Shooting toka mkoani Pwani dhidi ya Costal Union toka mkoani Tanga.
Matokeo ni kwamba timu ya Ruvu Shooting imepata ushindi wa bao moja kwa sifuri.

RATIBA YA UEFA CUP HII HAPA

Klabu ya Liverpool itakutana na klabu ya Ureno, Benfica katka hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa League, wakati klabu ya Fulham itakutana na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Ujerumani, Wolfsburg.Liverpool, ambayo ilijikuta ikitua katika mashindano haya baada ya kutolewa katika hatua ya kwanza ya mtoano baada ya kutolewa katika ligi ya mabingwa, walikata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuichapa klabu ya Ufaransa, Lille 3-1 kwa magoli ya Jumla. Liverpool na Benfica wanarekodi ya kushinda mara saba UEFA CUP.
Fulham, ushindi iliyoupata wa magoli 4-1 dhidi ya klabu kongwe ya Serie A, kibibi kizee cha Turin Juventus na kusonga mbele kwa jumla ya magoli 5-4, sasa itakutana na Wolfsburg, timu nyingine ambayo iliondolewa katika hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa.
Robo fainali zingine mbili, Hamburg ambayo uwanja wake ndiyo utakaotumika kwa fainali za mwaka huu, Hamburg Arena, watakutana na Standard Liege ya Ubelgiji, na huku klabu za Hispania zikiuana zenyewe kwa zenyewe yaani Valencia na Atletico Madrid.
Michezo ya kwanza ya robo fainali imepangwa kuanza kupingwa April 1, huku michezo ya marudiano ikipigwa April 8.
Michezo ya nusu fainali itachezwa kati ya April 22 na 29, huku fainali ikipigwa siku ya Jumatano katika uwanja wa Hamburg Arena hapo May 12.

ratiba kamili ya UEFA CUP

Fulham v Wolfsburg

Hamburg v Standard Liege

Valencia v Atletico Madrid

Benfica v Liverpool

RATIBA YA LIGI YA MABINGWA ROBO FAINALI HII HAPA

NYON, Switzerland
Klabu ya Arsenal itaikabili Barcelona katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya katika hatua ya robo fainali, ikiwa historia ya inajirudia tena kwani walikwishawahi kukutana mwaka 2006 ambayo Barca alifanikiwa kuibuka mbabe.Manchester United, ambayo ilichapwa na Barcelona katika mchezo wa fainali mwaka jana, sasa Man itacheza na Bayern Munich, wakati Inter Milan yenyewe itacheza na CSKA Moscow na Lyon imepangwa kucheza Mfaransa mwenzao klabu ya Bordeaux katika ratiba ambayo leo Ijumaa.
Michezo wa kwanza umepangwa kuchezwa March 30/31 huku mchezo wa marudiano ukichezwa April 6/7.
Ratiba ya nusu fainali pia imepangwa tayari, ambapo mshindi katika mchezo kati ya Man United na Bayern Munich atakutana na Lyon au Bordeaux, na mshindi kati ya Inter au CSKA atacheza na mshindi kati ya Arsenal au Barca.
Katika michezo ya robo fainali tayari Ufaransa imekwishajihakikishia kuwa na timu moja katika hatua ya Nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu klabu ya Monaco ifanikiwe kutinga hatua hiyo mwaka 2004.
Kwa klabu ya Arsenal ratiba imempa nafasi ya kulipa kisasi cha kutolewa na vijana hao wa Hispania, Barcelona 2-1 walipokutana katika dimba la Stade de France jijini Paris miaka minne iliyopita.
The Gunners wamefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali wakiwa na rekodi ya kumchapa Porto nagoli 5-0 na kusonga mbele kwa jumla ya magoli 6-2, utakumbuka mdau wa viwanjani, Porto iliwahi kutwaa ubingwa huo mwaka 2004.
Kikosi cha Mzee Arsene Wenger, kitakuwa kikisaka ushindi wake wa kwanza barani Ulaya.
Mabingwa mara tatu wa michuano hii, Manchester United kwa mujibu wa ratiba sasa wanatakiwa kunoa upya mapanga yao, kwani wanakutana na Bayern, utakumbuka waliwahi kukutana huko Camp Nou na Man kukfanikiwa kutwaa ubingwa mwaka 1999.
Lakini miaka miwili baadae, Bayern iliichapa Man United katika hatua ya robo fainali na kufanikuiwa kulitwaa kombe.
Msimu huu fainali zitapigwa katika uwanaja wa Real Madrid, Dimba la Santiago Bernabeu hapo May 22, itakuwa ni mara ya kwanza fainali za ligi ya mabingwa kuchezwa siku ya Jumamosi.
Ratiba ya hatua robo fainali.

Lyon (FRA) v Bordeaux (FRA)

Bayern Munich (GER) v Manchester United (ENG)

Arsenal (ENG) v Barcelona (ESP)

Inter Milan (ITA) v CSKA Moscow (RUS)

Mchezo wa kwanza utapigwa March 30/31

michezo ya marudiano itapigwa April 6/7

WAFAHAMU WAPINZANI WA SIMBA LEO


Klabu ya Lengthens Football Club ilianzishwa mwaka 2002 baada ya kununuliwa ikiwa daraja la pili ambapo ilikuwa ikifahamika kama Black Eagles. Lengthens Football Club – jina lake la utani ni “The Happy People” ama watu wenye furaha – ilifanikiwa kupanda kucheza ligi kuu mwaka 2007.
ikiwa ni mwaka wake wa tatu katika ligi kuu, Lengthens tayari imekwishafanikiwa kutwa ubingwa wa BancABC Sup8r.
Mwaka 2008, Lengthens ilifanikiwa kucheza fainali katika michuano hiyo lakini ilifungwa na Caps United.

Safari ya Lengthens hata hivyo imeanza mbali hata kabla ya mwaka 2002. Asili ya klabu hiyo inakumbukwa toka wakati wa ligi ya Kanda ya Kuwadzana wakati klabu hiyo ilipokuwa ikiundwa na vijana wadogo ambapo walikuwa wakicheza kama sehemu ya burudani tu.
Nje ya soka na majukumu ya kijamii, klabu hii, ilipewa jina la Young Pirates na kufanikiwa kutwaa tuzo mbali mbali. Baada ya mafanikio hayo ndipo viongozi walipoamua sasa kuitazama katika mafanikio zaidi na soka la kulipwa ambalo linaushindani zaidi na ndipo walipoamua kuiingiza katika ligi.
Viongozi wake ndipo walipoamua kuinunua klabu ya ligi daraja la pili na kufanikiwa kuipandisha daraja hadi ligi kuu mwishoni mwa msimu wa mwaka 2006.
Lengthens Football Club siku zote imekuwa ni klabu yenye mafanikio na inakumbukwa mwaka 2003 “The Happy People” walifanya vizuri kiasi cha kutamba katika michuano ya ZIFA Unity Cup.
Hata hivyo Lengthens Football Club katika michuano hiyo ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Dynamos.
Mwaka 2006, Lengthens ilifanikiwa kutinga hatua ya pili ya michuano ya CBZ Unity Cup baada ya kuifunga CAPS United lakini ilipoteza dhidi ya Buymore kwa mikwaju ya penati.
Mwaka 2007, Lengthens ilimaliza ikiwa miongoni mwa timu nane za juu katika ligi na mwaka uliyofuata katika michuano ya Sup8r, ambapo walipoteza mchezo dhidi ya Caps United. Mwaka 2008, Lengthens ilimaliza ikiwa miongoni mwa timu nne za juu na pia ilishiriki tena katika michuano ya Sup8r, kombe ambalo walifanikiwa kulitwaa kwa mara ya kwanza katika ligi.
Lengthens ama The Happy People inanolewa na kocha Mandla Masuku wakati meneja wa timu ni Robert Matoka. Mussa Gwasira ni raisi wa klabu na patron wa Lengthens Football Club. Mwenyekiti wa Lengthens ni Irvin Mereki wakati katibu mkuu ni John Chikochi.
Plaxedes Masenda ni shabiki nambari moja wa Lengthens Football Club.
Makocha waliyowahi kuifundisha klabu ya Lengthen FC ama “The Happy People” ni pamoja na Moses Chunga, Bigboy Mawiwi na marehemu Vusa Mlilo.
Makocha wengine ni pamoja na Gilbert Mapemba ambaye sasa anaifundisha klabu ya Caps United, Ephraim Mazarura sasa anaifundisha klabu ya Dynamos, Tendayi Nyamadzawo sasa yupo Caps United na Felix Kuswatuka ni miongoni mwa wachezaji ambao wanarekodi nzuri na kiwango cha hali ya juu ambao waliwahi kutamba na Lengthens.
Kauli mbiu ya Lengthes fc ni “If God is for us, who can be against us - The Happy People”

SIMBA DIMBANI LEO ZIMBABWE


KIKOSI CHA SIMBA
Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Wekundu wa Msimbazi Simba IJUMAA wanashuka dimbani huko HARARE kukipiga na Lengthens ya Zimbabwe mchezo utakaopigwa kwenye dimba la RUFALO lililopo eneo maarufu la MBARE kilomita 13 kutoka kwenye hotel ya CREASTER waliofikia Wekundu hao.

Wekundu hao huenda wakamkosa beki wake wa kushoto Juma Jabu ambaye ana maumivu ya kisigino na ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake.

Simba wamefanya maandalizi yao ya mwisho leo asubuhi na wakiwa tayari kwa pambano hilo la kesho litakakalochezwa saa kumi jioni kwa Zimbabwe ambayo itakuwa saa 11 jioni kwa nyumbani TANZANIA.

Tayari nahodha wa wekundu hao Nico Nyagawa amekwishaweka bayana kuwa hapo kesho kwa dua na sala za waTanzania ushindi upo.
KIKOSI CHA LENGTHES FOOTBALL CLUB

Simba na Lengthens ni kama wanafungua njia Huko Zimbabwe ikiitwa wiki yenye shamrashamra za soka kwani hapo Jumamosi nako kuna mchezo mwingine utakaowakutanisha GUNNERS dhidi ya Al Ahly ya Misri na hapo Jumapili CAPS UNITED watashuka dimbani kuwakaribisha MOROKA SWALLOS ya AFRICA KUSINI mechi zote zikipigwa kwenye dimba hilo la RUFARO.

MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI SIMBA SPORTS CLUB

MKWASA: TWIGA STARS ITAWAFUNGA ETHIOPI, NJOONI JUMAMOSI MUONE


Kocha mkuu wa Timu ya taifa ya wanawake Twiga Starz inayojiandaa na mchezo wake wa marudiano na Ethiopia wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Africa Charles Boniface Mkwasa amesema maandalizi yanaendelea vizuri kuelekea mchezo huo utakaopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa UHURU.

Mkwasa amesema vijana wake wapo sawa sawa na wapo tayari kwa mchezo huo wa Jumamosi.
Aidha Mkwasa amewataka mashabiki wa kandanda Tanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo kuwapa sapoti wanawake na siyo kusubiri hadi pale timu ya taifa ya wanaume inapocheza.
Amesema michango ya hali na mali inayotolewa itakuwa na faida kubwa endapo itaongezewa na morari wa mashabiki kufurika uwanjani na kuwashangilia wanawake wanaoliwakilisha taifa katika michuano ya kimataifa ya kufuzu kucheza mataifa ya Afrika kwa upande wa wanawake.

Thursday, March 18, 2010

TEGETE AKWEA PIPA KWENDA SWEDEN


Tegete amekwea pipa kuelekea nchini Sweden huku tayari Taifa Starz ikiwa imeingia kambini kujiandaa na mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali za mataifa bingwa barani Africa CHAN dhidi ya SOMALIA,mchezo utakaochezwa Jumamosi ya March 27 kwenye uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa NDUMBARO SOCCER AGENCY DAMAS NDUMBARO amesema Tegete atakuwa kwenye majaribio mpaka mwishoni mwa mwezi huu.
Tegete anatarajiwa kurejea nchini tarehe 31 ya mwezi huu kabla ya kupigwa mchezo kati ya Simba na Yanga.

ZAIN KUDHAMINI MAONYESHO YA WASANII WENYE VIPAJI NA UBUNIFU

Mkurugenzi wa Andika Afrika Publishers, Neema Kambona akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya Tamasha la wasanii wenye vipaji na ubunifu litakalofanyika jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 20,2010 katika ukumbi wa Nafasi Art Space Mikocheni . Tamasha hilo limedhaminiwa na kampuni ya Simu za mkononi ya Zain Tanzania.

Sauda Simba kutoka Trinity Promotion (katikati) akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam juu ya Tamasha la wasanii wenye vipaji na ubunifu litakalofanyika Jumamosi Machi 20, 2010 katika ukumbi wa Nafasi Art Space Mikocheni Dar es Salaam. Tamasha hilo linadhaminiwa na kampuni ya Simu za mkononi ya Zain Tanzania. Kulia ni Meneja uhusiano wa Zain Muganyizi Mutta na kushoto ni Fred Halala kutoka Nafasi Art Space.

Mratibu wa Tamasha la wasanii wenye vipaji na ubunifu litakalofanyika jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 20, 2010 katika ukumbi wa Nafasi Art Space Mikocheni jijini Evans Bukuku (kushoto) akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam juu ya maandalizi ya Tamasha hilo ambalo limedhaminiwa na kampouni ya Zain Tanzania. Wengine ni Muganyizi Mutta wa Zain na Sauda Simba wa Trinity Promotion.

Mtaalam wa kuchonga vinyago Mwandale Wakwenya akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya kazi zake atazoonyesha wakati wa Tamasha la Wasanii wenye vipaji na ubunifu litakalofanyika Jumamosi Machi 20,2010 katika ukumbi wa Nafasi Art Space Mikocheni Dar es Salaam. Tamasha hilo limedhaminiwa na kampuni ya Zain Tanzania. Kushoto ni Neema Kambona kutoka Andika Africa Publishers.


Kampuni ya simu za mikononi Zain kudhamini maonyesho ya wasanii wenye vipaji na ubunifu.
Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania inadhamini maonyesho ya wasanii wenye vipaji mbali mbali kama vile muziki, uchoraji, utunzi na vipaji vinginevyo, yatakjayofanyika jumamosi machi 20 katika ukumbi wa Nafasi Art Space Mikocheni nyuma na Fiesta Pub jijini Dar es Salaam.
Maonyesho hayo yatawapa nafasi wasanii kuonyesha vipaji vyao na pia kuonyesha kazi zao mbali mbali za kisanaa.
Washiriki katika maonyesho hayo ni wahitimu wa kozi mbali mbali za kisanaa waliomaliza mafunzo mwaka 2009. Jumla ya wasanii 60 walishiriki kozi hiyo chini ya udhamini wa Balozi wa Denmark na British Council, kama sehemu yao ya kusaidia sekta ya ubunifu.
Kati ya washiriki wa maonyesho hayo ni mwandale Mwanyekwa ambaye ni mchongaji maarufu wa vinyago anayefahamika kitaifa na kimataifa kwa ubunifu wake wa kipekee, Mwanamitindo Kemy Kalikawe, Mwanamitindo Chipukizi Naledi Label, pamoja na Sauda Simba ambaye atakuwa akizindua wimbo w ake wa "SAUTI YA SAUDA". Huu ni wimbo wa pili na unafuatia mafanikio ya Alkbamu yake ya kwanza maarufu ya "SIMPLY JAZZMIN".
Wengine ni mtayarishaji wa muziki maarufu Ambrose Akula Akwabi a.k.a DUNGA ambaye alishiriki katika kutengeneza nyimbo ambazo zimewahi kutamba sana kama vile ANITA wa MATONYA, Mr Politician ya NAKAAYA, NIpe Deal ya Ngwear na wengineo wengi.
Maonyesho yataanza saa nne Asubuhi. Watoto pia watakuwa na nafasi ya kufurahi na wanamuziki mbalimbali kama vile Daz, Ngoma Afrika, Sauda Simba na kuangalia picha mbali mbali zitakazoonyeshwa na wataalam wa picha wa World Pictures (WAPI) ambao wamekuwa waikishirikiana na British Council kuandaa tamasha kama hili ambalo kwa sasa ni tamasha la tatu.
Meneja mawasiliano wa Zain Tanzania Beatrice Singano amesema Zain Tanzania imefurahi kudhamini maonyesho haya ili kuwasaidia wasanii wa Tanzania kuonyesha vipaji vyao na kujitangaza, jambo ambalo litawasaidia kufahamika katika soko na kujiendeleza.

Wednesday, March 17, 2010

CHELSEA YATOLEWA MABINGWA ULAYA

Chelsea imeondolewa katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya vijana wa Jose Mourinho, Internazionale kuibuka na ushindi wa goli 1-0 katika dimba la Stamford Bridge na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwa jumla ya magoli 3-1.
Inter imekuwa ikitolewa katika hatua ya mtoano ambayo hujumuisha klabu 16 katika ligi ya mabingwa barani Ulaya katika kipindi cha misimu mitatu mfululizo, tena ikiotolewa na klabu za Uingereza mara mbili, lakini Samuel Eto'o kunako dakika 79 ilitosha kuwaondosha Chelsea nje ya ligi ya mabingwa.
Didier Drogba alijikuta akitolewa kwa kadi nyekundu dakika tatu kabla ya mpira kumalizika kufuatia kumchezea Thiago Motta.
Makocha wote wawili walifanya mabadiliko, kocha Mourinho alimuingiza Goran Pandev na kufanya safu ya ushambuliaji kuwa na wachezaji wa tatu ikiwa ni pamoja na Eto'o na Diego Milito, wakati Carlo Ancelotti alimuingiza mlinzi Paulo Ferreira pamoja na Yuri Zhirkov.
Golikipa nambari tatu wa Chelsea Ross Turnbull alikaa golini ikiwa ni mchezo wake wa tatu akiwa amaevalia jezi ya Chelsea.
Mdau wa viwanjani anawapa Pole mashabiki wa Chelsea na kuwapongeza mashabiki wa Inter MilanDidier Drogba akimuomba msamaha Mwamuzi baada ya kumlima kadi nyekundu.Makocha kazini, Morinho naye anambwembwe?

Tuesday, March 16, 2010

SIMBA WANYIMWA HOTELI ZIMBABWE

Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa wekundu wa msimbazi simba, wamewasili salama wa salamini huko mjini Harere nchini Zimbabwe tayari kwa pambano lao la mwishoni mwa juma hili dhidi ya wenyeji wao Lengthens.
Akizungumza na Michezo na Times meneja wa kikosi cha wekundu hao Inocent Njovu amesema safari yao toka nchini Tanzania ambayo ilianza majira ya alfajiri ilikuwa salama na wamewasili mjini Harare mishale ya saa saba mchana ambapo kwa ukanda wa Afrika mashariki ilikuwa mishale ya saa nane alasiri.
Njovu amesema pamoja na kuwasili salama huko mjini Harare nchini Zimbabwe, mpaka mishale ya jioni walikua bado hawajapatiwa sehemu ya malazi ambayo ilistahili kuandaliwa na wenyeji wao.
Wakati wawakilishi hao pekee wa Tanzania wakiwasili huko nchini Zimbabwe tayari kwa pambano lao la mwishoni mwa juma hili, hapa nyumbani shirikisho la soka nchini TFF kupitia kwa katibu wake mkuu Fredrick Mwakalebela limewatakiwa kheri wawakilishi hao.
Njovu amesema kiongozi wa msafara ambaye anatoka shirikisho la kandanda Tanzania TFF Msafiri Mgoi anafuatilia suala hilo la wao kuwekwa nje jambo lililowalazimu wachezaji kuacha mabegi nje ya hoteli na kwenda mazoezini huku wakiwaacha viongozi wakifuatilia mustakabali wa wapi watalala.

TAIFA STARS IMEINGIA KAMBINI TAYARI KUIKABILI SOMALIA

Timu ya soka ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS hii leo imeingia kambini tayari kwa kuanza maandalizi ya mchezo wake wa kufuzu kucheza fainali za mataifa bingwa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN dhidi ya timu ya taifa ya Somalia.
Taarifa za kuingia kambini kwa timu hiyo, zimetolewa na katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF Fredrick Mwakalebela alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Mwakalebela amesema kwa ujumla timu italigharimu shirikisho la soka nchini TFF shilingi million 40 katika kipindi hichi cha maandalizi mpaka siku ya mchezo dhidi ya Somalia ambao utachezwa March 28.
Aidha mwkalebela amezungumzia maamndalizi ya timu nyingione za taifa za Tanzania ambazo pia zinajiandaa na michezo yake ya kimataifa ambapo kwa upande wa timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars inajiandaa na mchezo wake wa marejeano dhidi ya Ethiopia huku timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ambayo inajiwinda na mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Malawi.

ULINZI STARS YASHIKILIA USUKANI WA LIGI KUU KENYA

Klabu ya Kenya, Ulinzi Stars, ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa msimu wa ligi kuanza, sasa inaongoza ligi kuu ya Kenya (Kenya Premier league) ikiwa na jumla ya pointi 10, ikiwa pointi moja mbele dhidi ya KCB ambayo imefanikiwa kushinda michezo mitatu na kupoteza mchezo mmoja.
Klabu ya Western Stima inashika nafasi ya tatu ikiwa na jumla ya pointi 8, moja zaidi ya timu inayoshika nafasi ya nne klabu ya Sher Karuturi na pointi mbili mbele ya klabu kongwe ya Tusker na kukamilisha klabu tano ambazo zimekuwa na matokeo mazuri tangu kuanza kwa ligi.
Mathare United ilipata ushindi wake wa kwanza msimu huu katika mchezo wa jumapili kwa kuifunga Posta Rangers 2-1 na kujikuta ikilala nafasi ya sita ikilingana pointi na Tusker pamoja na Nairobi City Stars, Sony Sugar na AFC Leopards ambao wanashika nafasi ya 7 hadi 9 katika msimamo.
Mabingwa watetezi, klabu ya Sofapaka, ambao walipata pointi katika mchezo wa jumatatu dhidi ya Mahakama, sasa inashika nafasi ya 10 katika msimamo ikiwa na pointi nne.
Nafasi ya 11-13 inashikiliwa na Mahakama, Gor Mahia na Thika United ambazo zinapointi tatu kila moja, wakati Chemilil Sugar na Posta Rangers zinapointi moja moja na kushika nafasi ya 14 na 15.
Klabu ya Red Berets inashikilia mkia wa ligi kuu ya Kenya wakiwa na pointi moja mkononi.

Monday, March 15, 2010

CHUO KIKUU CHA AFRICA NAZARENE CHANG`ARA AFRICA CHALLENGE DHIDI YA NJALA CHA SIERRA LEONE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

March 15, 2010

Chuo kikuu cha Kenya cha Africa Nazarene chang’ara Zain Africa Challenge dhidi ya Chuo kikuu cha Njala cha Sierra LeoneChuo kikuu cha Africa Nazarene kutoka Kenya kimeng’ara katika mashindano ya Zain Africa Challenge baada ya kuwashinda wapinzani wao Chuo Kikuu cha Njala kutoka Sierra Leone katika mashindano ya Vyuo vikuu ya Zain Afrika Challenge (ZAC) yaliyofanyika jumapili saa tatu usiku na kuonyeshwa moja kwa moja kupitia luninga ya TBC 1.
Africa Nazarene ambao walionesha umahiri mkubwa katika kujibu maswali kwa haraka haraka walipata jumla ya pointi 920 huku wapinzani wao Njala wakiambulia pointi 550.
Kufuatia ushindi huo Chuo Kikuu cha Africa Nazarene wataungana na wenzao katika raundi ya pili ya mtoano wa ZAC ambao ni chuo Kikuu cha Makerere ambao waliwashinda Chuo Kikuu cha Malawi katika ufunguzi wa mashindano hayo, pamoja na Chuo kikuu cha Ghana ambao waliwashinda Chuo kikuu cha Arusha cha Tanzania.
Vyuo Vikuu 16 vinachuana kuwania kitita cha dola za Marekani USD 50,000 pamoja na Kombe la Zain, ambayo ndiyo zawadi ya mabingwa katika msimu huu wan ne wa ZAC. Wanafunzi wa chuo kitakachoshinda watakaoshiriki katika mtoano huo pia kila mmoja wao atandoka na dola za Mareka USD 5000.
Kwa mwaka huu Tanzania inawakilishwa na Vyuo Vikuu viwili ambavyo ni Chuo Kikuu cha Tumaini pamoja na Chuo Kikuu cha Arusha. Hata hivyo Arusha tayari wamekwishatolewa, na kuwafanya watanzania sasa kuomba duha ya ushindi kwa Chuo kikuu cha Tumaini ili kiweze kufanya vizuri.
Programu ya Zain Afrika Challenge ni sehemu ya juhudi za Zain zinazolenga kuboresha sekta ya elimu na inadhihirisha dhamira ya Zain ya kuleta Ulimwengu Maridhwawa kwa wateja wa Zain.
Mwaka huu pia watazamaji wa Zain Afrika Challenge wanafursa ya kushiriki katika mchezo wa Zain kupitia SMS. Wateja wa mitandao yote nchini safari hii wataweza kujibu maswawali yanayoulizwa wakati na mtoani na kujishindia zawadi nono ambazo ni pamoja na simu mpya za mkononi aina ya Nokia N97 zenye thamani ya zaidi ya shilingi laki nane. Kushiriki katika mchezo wa ZAC watu wenye simu za mkononi watatuma majibu ya swali litakaloulizwa kwenda 15315. Zawadi hizi zitatolewa kila wiki ambapo watachaguliwa washindi watatu kila wiki.
Timu 100 kutoka Vyuo Vikuu vinavyoongoza kutoka nchi nane za Afrika ambazo ni; Tanzania, Ghana, Kenya, Malawi, Nigeria, Sierra Leone, Uganda na Zambia zilichuana katika mashindano ya awali ya kitaifa ili kutafuta nafasi ya kuwakilisha nchi zao katika mtoano wa kimataifa na kujipatia fursa ya kujishindia sehemu ya zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja (Dola za Marekani 1,000,000).
Kati ya timu hizo 100, timu 32 zilizoongoza zimefuzu kushiriki katika mashindano ya kimataifa yanayofanyika nchini Uganda katika ushindani wa hali ya juu ili kuwania nafasi ya kushiriki fainali ya mashindano ambayo yatarushwa na luninga katika nchi zote nane zinazoshiriki na pia kwa mara ya kwanza, mashindano haya yatarushwa Afrika nzima kupitia satellite ya DSTV na yatatazamwa na zaidi ya watu milioni 700 kila Jumatatu saa moja na nusu usiku kuanzia Machi 1, 2010 kwenye kituo cha Africa Magic.
Chuo Kikuu cha Makerere cha Uganda kiliuwa chuo kikuu cha kwanza kushiriki katika mashindano hayo yanayo rushwa kwa muda wa wiki 16 kikichuana na Chuo Kikuu cha Malawi.
Katika msimu wa tatu wa Zain Africa Challenge uliofanyika mwaka jana Chuo Kikuu cha Ibadan cha Nigeria kiliibua na ushindi katika mtoano huo wa chemsha bongo na kujinyakulia zaidi ya milioni 60 (USD 50, 000) kutoka Zain, wakati kila mshiriki alijipatia kitita cha dola za Marekani 5000 kila mmoja. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Chuo Kikuu cha Kenyatta ambacho kiliondoka na dola za Marekani 35,000, na kila mshiriki dola 3,500. Vyuo vingine vyote vilivyoshiriki vilipata zawadi zenye thamani kati ya dola 5000 na dola 25,000.
Maswali katika mtoano wa ZAC yanagusa maeneo mbali mbali ikiwemo, historia, sayansi, utamaduni wa Africa, Jiographia, literature, muziki ya matukio ya wakati huo. Kadhalika ZAC huonyesha fursa zilizopo za kielemu katika Vyuo Vikuu vya Afrika kupitia video na wasifu wa wanafunzi.
Jumapili ijayo Mabingwa wa ZAC mwaka 2009 Chuo Kikuu cha Ibadan watapambana na Chuo Kikuu cha Masomo ya Maendeleo cha Ghana.

Yatakayojiri ZAC Msimu wa nne

• Kwa mara ya kwanza kutakuwa na mshindano kwa njia ya mtandao kupitia ;www.facebook.com/ILoveZainAfricaChallenge na kutakuwa na zawadi za kila wiki za dola 100 katika muda wa maongezi na zawadi ya juu itakuwa Laptop.

• Kila wiki watu watapiga kura Barani Afrika kuchagua Mchezaji wa Wiki wa Mchezo na zawadi yake ni dola za Marekani 1000.

• Watazamaji watajishindia zawadi za juu ambazo ni pamoja na simu mpya aina ya Nokia zenye intaneti, muziki na video kwa kutuma majibu ya maswali yatakayoulizwa kwenda namba 15315.

• Zain Africa Challenge sasa inajumuisha watu wetu zaidi licha ya wachezaji, watu wa Idara ya Utawala katika Vyuo Vikuu na wanavyuo kwa sababu sasa taarifa zake zinapatikana kwenye Facebook na Twitter.

OKWI, NYOSO WAACHA SAFARI YA WAZIMBABWE

MSHAMBULIAJI wa kulipwa wa timu ya Simba, Mganda, Emmanuel Okwi na beki wa kutumainiwa Juma Nyoso wameachwa katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza na Lengthens FC Machi 19 jijini Harare.
Simba imeondoka leo alfariji kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya ikiwa na msafara wa watu 25, ambapo wachezaji ni 19 na viongozi sita kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho CAF dhidi ya Wazambabwe hao.
Akizungumza Dar es Salaam, Ofisa Habari wa timu hiyo, Cliford Ndimbo alisema Okwi ameachwa kutokana na kuwa mgonjwa lakini Nyoso hayumo katika orodha hiyo kutokana na nafasi.
"Wachezaji walioachwa si Nyoso na Okwi pekee kwani wapo wachezaji wengine wameachwa kutokana na idadi ya watu ambao wanahudumiwa na wapinzani wetu," alisema Ndimbo.
Ndimbo aliwataja wachezaji wanaokuwa katika msafara huo ni Juma Kaseja, Haruna Shamte, Juma Jabu, Nicco Nyagawa, Kelvin Yondani, Mohamed Banka, Hilary Echessa na Ramadhani Chombo.
Wengine ni Mussa Hassan Mgosi, Mike Barasa, Ulimboka Mwakingwe, Ali Mustapha, Salumu Kanoni, david Naftar, Uhuru Selemani, Jerry Santos, Mohamed Kujuso, Jabir Aziz na Joseph Owino.
Kwa upande wa viongozi watakaoambatana na timu hiyo ni Mwenyekiti Hassan Dalali, Kocha Patrick Phiri na Msaidizi wake Amri Said, Meneja Innocent Njovu, Daktari Cosmas Kapinga, Kassimu Dewji na Mulamu Ng'ambi.
Ndimbo alisema kikosi hicho kinaondoka kikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri kutokana na kufanya maandalizi ya kutosha wa ajili ya michuano hiyo.
Simba wanatarajia kurudi nchini mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo au JUmapili wakitegemea na ratiba ya ndege wanayosafiri nayo.

ZAIDI YA MILIONI MOJA WAJIUNGA NA NIPE NIKUPE YA ZAIN

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

ZAIDI YA MILIONI MOJA WAJIUNGA NA NIPE NIKUPE YA ZAIN

Dar es Salaam Machi 14, 2010

Zaidi ya wateja milioni moja wamejiunga na ofa mpya ya Zain ya Nipe Nikupe iliyozinduliwa Januari 28 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania, Khaled Muhtadi.Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania Muganyizi Mutta amesema katika taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam kwamba wateja wa Zain wanotumia ofa ya nipe nikupe ya kwanza ya aina yake Barani Afrika sasa wamefika milioni moja.
“Wateja wetu walikuwa wanataka unafuu wa kuongea na sasa wamepata. Zain inawarudishia wateja walio katika mpango wa Malipo Kabla pesa yote waliyotumia kupiga simu kutoka mtandao wa Zain kwenda mtandao wowote ule nchini siku hiyo hiyo papo papo, siyo kesho, wala kesho kutwa. Ni huduma ya Kipekee Barani Afrika na haina mpinzani,’’ alisema Mutta.
‘’ Tumeweka rekodi ya kuwarudishia mara mbili muda wa maongezi wateja wetu na hii ni kwenda mtandao wowote ule kuwaongezea muda wa kuwasiliana kupitia Nipe Nikupe ofa ya kwanza ya aina yake nchini Tanzania, ” alisema Mutta.
Wateja wa Zain walio katika mpango wa Malipo Kabla nchini kote wanarudishiwa Tsh 200 papo kwa papo kwa kila Tsh 200 wanayoitumia kila siku kupiga simu kutoka mtandao wa Zain kwenda mtandao wowote ule wa simu za mkoni nchini Tanzania ili mteja aendelee kupiga simu kwenda Zain au simu kwenda mtandao mwingine nchini.
“Tungependa wateja wetu wote wa Malipo Kabla wajiunge na Nipe Nikupe ili wanufaike na ofa hii ambayo haina mpinzani nchini Tanzania, ” alisema Mutta na kuongeza kwamba nipe nikupe imeanzishwa kuwazawadia wateja wa Zain kwa uaminifu wao na kwa kuichagua Zain kuwa mtandao wao wa mawasiliano na kuifanya kuwa mtandao Unaoheshimika zaidi Tanzania.
Kujisajili katika nipe nikupe, mteja anatuma SMS neno NIPE mara moja tu kwenda namba 15444, gharama za kujisajili ni ths 500 ambazo zinatozwa mara moja tu mteja anapojiunga. Kuangalia bonasi zake mteja anapiga *102#. Muda wa maongezi wa bonasi unaisha saa sita usiku siku hiyo hiyo.

MPIRA WA MIKONO NA MATUMAINI YA UBINGWA WA AFRIKA

Timu ya wanawake wa Tanzania ya mpira wa mikono, imepewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa michuano maalum ya Afrika mashariki na kati *Kombe la Challenge* itakayoanza kutimua vumbi lake April 29-May 5 mwaka huu huko nchini Djibouti.
Nafasi hiyo kwa timu ya Tanzania imetolewa na katibu mkuu wa Chama cha mpira wa mikono hapa nchini TAHA, Nickolaus Mihayo alipozungumza na Michezo na Times ambapo amesema mpaka sasa timu hiyo inajiandaa vyema.
Hata hivyo Mihayo amesema timu ya Tanzania itaundwa na wachezaji kutoka Tanzani bara na visiwani ambao watatangazwa hivi karibuni.

TBF WAAHIDI MAJIJI KURUDI NA UBINGWA WA KIKAPU TOKA MOMBASA, KENYA

Katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini TBF Alexender Msofe amesema wameandaa mikakati mizito ya kuzisaidia timu za majiji ya Tanzania ili ziweze kufanya vyema kwenye michuano ya majiji inayotarajia kuanza March 22 katika jiji la Mombasa nchini Kenya.
Akizungumza na Michezo na Times Msofe amesema kwa mwaka huu wana imani timu za majiji ya Tanzania zitafanya vyema na kufika mbali kwenye michuano hiyoa mbayo hufanyika kila mwaka.
Msofe ametanabai kuwa imani hiyo ya timu hizo kufanya vyema mwaka huu imekuja kufuatia wao kama viongozi wa TBF kupata taarifa nzuri za maandalizi kutoka kwa viongozi wa vyama mikoa inakayounda timu za majiji.

YANGA YAPEWA SIKU 14 KUITISHA MKUTANO MKUU, MADEGA AJIBU MAPIGO AWATAKA WAJEE KATIKA KATIBA YA YANGA

BARAZA la wadhamini wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam limeulima barua uongozi wa klabu hiyo, likiuagiza kufanya mambo mbalimbali ili kuboresha klabu hiyo ukiwemo Mkutano Mkuu ndani ya siku 14 tangu Ijumaa iliyopita.
Kwa mujibu barua ambayo baraza hilo limemwandikia Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Imam Madega na kunaswa na vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na gazeti la majeri na Radio Times FM 100.5 hili kufanikiwa kunasa nakala yake, baraza hilo linamtaka kuitisha huo mkutano huo, ili kufanya marekebisho ndani ya Katiba kama inavyotakiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Baraza hilo limesema kuwa ni lazima mkutano huo ufanyike ndani ya siku 14 na mapendekezo ya mabadiliko ndani ya katiba ni lazima yatangazwe hadharani kwa muda wa wiki moja, kabla ya kuidhinisha, ili kuweza kuwashirikisha wanachama katika kuamua jambo hilo.
"Na baada ya marekebisho kupitishwa unapaswa kuyafuata na kuyaingiza ndani ya katiba haraka iwezekanavyo na inapaswa kufahamu kazi hii, inatakiwa isichukue muda zaidi ya wiki mbili," ilielza sehemu ya barua hiyo.
Mbali na Mkutano Mkuu na marekebisho ya katiba, baraza hilo limemwagiza Katibu Mkuu na Kamatai yake ya Sekeretarieti kuhakikisha inawakilisha ripoti ya kumbukumbu za mahesabu zilizohakikiwa katika kipindi chote cha uongozi wa mwenyekiti huyo.
Pia baraza hilo limemtaka Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Kostadin Papic kuandaa taarifa za kipindi atakachokuwa ameionoa klabu hiyo, ili kuepukana na tatizo kama la kocha aliyefundisha timu hiyo msimu uliopita na kisha kuondoka bila kuandika taarifa.
"Kwa uwezo wangu kama mdhamini, nitahitaji nakala ya ripoti zote kuwakilishwa katika Baraza la Wadhamini, pamoja na ajenda zake walau siku saba kabla, ili niweze kufanya tathimini kama mdhamini wa Yanga," ilieleza barua hiyo.
Barua hiyo ambayo ilisainiwa na mmoja wa wajumbe wa baraza hilo, ilieleza kuwa endapo mambo hayo yatakuwa yameenda kama inavyotakiwa, wanatarajia watakuwa wamepokea taarifa hizo Juampili ya Aprili 24, mwaka huu ambayo itakuwa ni muda wa wiki moja, baada ya mechi yao ya mwisho ya ligi.
Wadhamni hao pia wamemwagiza mwenyekiti, kuandaa taarifa muhimu katika magazeti na vyombo mbalimbali vya habari siku moja baada ya mkutano wa mabadiliko ya katiba kumalizika.
Katika barua hiyo wadhamini hao walisema endapo kutakuwepo masuala mengine yanayohitajika kupatiwa ufumbuzi, ili kuhakikisha Baraza la Wadhamni na Uchaguzi Mkuu unafanyika kama vile kuchagua kamati itakayoshughulikia uchaguzi itabidi yapatiwe ufumbuzi katika muda unaotakiwa.
Aidha michezo na Times FM ilifainikiwa kuzungumza na mwenyekiti wa Yanga Imani Madega ambaye amesema Baraza la wadhamini wa klabu hiyo halikuisoma vema katiba ya klabu hiyo na kusema kazi ya wadhamini katika klabu ni kusimamia masuala ya fedha.
Madega amesema hakuna chombo chochote katika klabu ya Yanga ambacho kitatoa maamuzi yeyote ya nini kifanyike kwa maana shughuli za kila ssiku za klabu ya Yanga zaidi ya mwenyekiti.

SIMBA BINGWA LIGI KUU TANZANIA BARA 2009/2010

Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imefanikiwa kutangaza ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuichapa timu ya Azam FC magoli mawili kwa bila katika mchezo uliyopigwa kunako uwanja wa Uhuru.
Shujaa wa Simba katika mchezo huo alikuwa mchezaji wa kimataifa wa Kenya Mike Barasa.
Kufuatia ushindi huo SImba inafikisha Jumla ya pointi 56 ambazo haziwezi kufikiwa na klabu yeyote katika ligi kuu Tanzania Bara.Klabu ya Yanga ambayo inashikilia nafasi ya pili, ikiwa na jumla ya pointi 45, hivyo hata ikishinda michezo yote itafikisha jumla ya pointi 54 hivyo kuwalazimu Simba kutangazA ubingwa mapema huku wakiwa wamebakiza michezo miwili kabla ya kumaliza ligi Kuu Tanzania Bara.

Sunday, March 14, 2010

GOFU YA LUGALO YAENDELEA KUNUFAIKA NA ZAWADI ZA ZAIN

Warui Mwangi (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa kapteni wa klabu ya gofu ya Lugalo, Samuel Hagu baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya gofu yaliyofanyika jumamosi katika viwanja vya gofu vya Lugalo jijini Dar es Salaam.Mchezaji gofu kutoka Zambia Goege Stuart akipiga mpira kuelekea shimoni, katika mashindano ya gofu yaliyofanyika katika viwanja vya gofu vya Lugalo jijini Dar es saalam jumamosi.Mchezaji gofu kutoka Zambia Kain Mbaya akijiandaa kupiga mpira wa gofu kelekea shmoni, katika mashindano ya gofu yaliyofanyika katika viwanja vya gofu vya Lugalo jana Dar es saalam.Alex Kiome (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa kapteni wa klabu ya gofu ya Lugalo, Samuel Hagu baada ya kuwabwaga zaidi ya wachezaji themanini na tano( 85) na kuibuka mshindi wa jumla, katika mashindano ya gofu yaliyofanyika jumamosi katika viwanja vya gofu vya Lugalo jijini Dar es Salaam.