Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, July 6, 2012

BANKA, MESHACKA ABEL NA WENGINE WA5 WAPATA ITC KUCHEZA KENYA, MSUMBIJI



 SHIRIhirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa Watanzania saba kucheza mpira wa miguu katika nchi za Kenya na Msumbiji.


TFF imetoa hati hizo kwa wachezaji hao baada ya kuombewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Msumbiji (FMF) ili waweze kucheza katika klabu za nchi hizo.


Wachezaji waliokwenda Bandari ya Kenya na klabu walizokuwa wakichezea nchini kwenye mabano ni David Naftali (huru), Meshack Abel (huru), Mohamed Banka (huru) na Thomas Mourice (Mtibwa Sugar).


Klabu ya CD Madchegde ya Msumbiji imewachukua wachezaji Hassan Hassan Mustapha kutoka Mgambo Shooting ya Tanga, na Abdallah Ally Abdallah na Thobias David Silas kutoka klabu ya daraja la kwanza ya Transit Camp ya Dar es Salaam.

NA ODHIAMBO WA AZAM APATA ITC
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya mchezaji George Odhiambo, raia wa Kenya aliyejiunga na klabu ya Azam.

Hati hiyo imetolewa na Chama cha Mpira wa Miguu cha Denmark (DBU) ambapo Odhiambo alikuwa akicheza nchini humo kabla ya kutua Azam kwa ajili ya msimu wa 2012/2013.

Klabu nyingine zinazosajili wachezaji kutoka nje ya Tanzania zinatakiwa kuhakikisha zinakamilisha uhamisho wao (transfer) kabla ya Julai 30 mwaka huu ambayo ndiyo siku ya mwisho kufanya hivyo.

Kanuni ya 41 ya Ligi Kuu kuhusu ITC inasema: “(1) Maombi ya ITC kwa wachezaji wa kigeni wa kulipwa yatawasilishwa kupitia mtandao wa kompyuta kwa kutumia program ya ‘Transfer Matching System-TMS’ baada ya klabu zinazohusika na mchezaji huyo au wachezaji hao kukubaliana nje ya mtandao.

(2) Maombi ya ITC kwa wachezaji wa kigeni wasio wa kulipwa yatawasilishwa kwa barua TFF baada ya klabu zinazohusika na mchezaji huyo au wachezaji hao kukubaliana. Chama cha Soka kinachotoa ITC kwa njia hii kitapeleka nakala FIFA. (3) ITC haihitajiki kwa mchezaji mwenye umri chini ya miaka kumi na mbili (12).”

Tunapenda kuzikumbusha klabu kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 53 ya Ligi Kuu, wachezaji wa kigeni ni lazima wawe wanachezea timu ya Taifa au klabu za Ligi Kuu huko wanakotoka.

Kanuni hiyo inasema: “Klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wa ngazi ya kimataifa ambao ni wa timu za Taifa na Ligi Kuu kutoka nje ya nchi wasiozidi watano (5). 

Wachezaji kutoka Ulaya na Marekani ya Kusini wanweza kuwa wa daraja la pili na kuendelea, na klabu inaruhusiwa kuchezesha wachezaji walioorodheshwa wasiozidi watano (5) wa kigeni katika mchezo mmoja. Wachezaji hao watasajiliwa baada ya TFF kuhakikisha usahihi wa taarifa zao na kukamilika kwa taratibu za uhamisho wa kimataifa.”

No comments :

Post a Comment