|
Meneja
wa bia ya Serengeti Lager Bw. Allan Chonjo kulia akikabidhi funguo za
gari aina ya Ford Figo kwa mshindi wa gari hiyo katika Promosheni ya
"Vumbua Dhahabu chini ya Kizibo" Bw. Isack Juvenary aliyojishindia hivi
karibuni kutoka mkoani Morogoro, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika
kwenye Duka la magari la CMC Motors lililopo katika barabara ya Azikiwe
jijini Dar es salaam, katika picha wanaoshuhudia tukio hilo ni maafisa
kutoka kampuni ya bia ya Serengeti |
|
Meneja
wa bia ya Serengeti Lager Bw. Allan Chonjoakizungumza na vyombo vya
habari mara baada ya kukabidhi gari hilo, kulia ni mshindi wa gari hilo
Isack Juvenary |
|
Isack
Juvenary akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya bia ya
Serengeti, wa tatu kutoka kushoto ni Meneja wa bia ya Serengeti Lager
Allan Chonjo |
|
Bw. Isack Juvenary akifurahia gari yake huku akiwa haamini kilichotokea. |
|
Bw. Isack Juvenary akifurahia gari yake huku akiwa amepozi pembeni mwa gari yake. |
Isack Juvenary mwenye umri wa miaka 25 mkazi Morogoro ambaye ndiyo mshindi wa gari mpya aina FORD FIGO,Leo asubuhi katika ofisi za CMC zilizopo barabara ya azikiwe mkabala na jengo la maktaba square jijini Dar Es Salaam, amekabidhi wa zawadi yake hiyo ya gari na kushuhudiwa na vyomvo mbalimbali vya habari.
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni ijulikanayo kama vumbua hazina chini ya kizibo. Promosheni hiyo inaendeshwa nchi nzima kwa
wateja mbalimbali wa kampuni hiyo kujishindia zawadi za kila aina
zikiwezo Magari. Bajaj, Pikipiki, Jenereta na zawadi zingine kemkem
Akiongea na wandishi wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hiyo, meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager Bw. Allan Chonjo amesema “Najisikia faraja kubwa sana ninapoona yale tuliyoyapanga kuyatimiza kwa wateja wetu kama SBL na kwamba hii ni sehemu tu ya yale yote tuliyopanga kufanya kwa jamii inayotuzunguka kwa kuthamini mchango wa wateja wetu
na pia sisi tumelenga katika kuwapa mabadiliko katika maisha yao kwa
kuzingatia mahitaji muhimu ya binadamu siku had siku.
Ndiyo maana tuna zawadi za
magari, Bajaji, majenerata na pikipiki ili ziwasaidie katika shughuli
zao za kila siku na pia fedha taslimu kuanzia shilingi elfu kumi, elfu
hamsini na laki moja ambazo unaweza kushinda” alisema Chonjo huku akisisitiza kuwa promosheni hiyo
bado inaendelea kwa wiki takriban saba zijazo na kuwataka watanzania
wote wenye sifa zilizoainishwa katika vigezo na masharti vya promosheni hiyo kushiriki kwa wingi ili kuongeza uwezo wakushinda zawadi mojawapo.
No comments :
Post a Comment