MTANDAO wa Wandishi wa Habari
nchini (TAJONET), umefanikiwa kupitisha rasimu ya Katiba ambapo kamati
iliyosimamia mchakato wa rasim hiyo, imekabidhiwa jukumu la kukamilisha usajili ndani ya wiki mbili.
Mwenyekiti wa Mtandao huo
Williamu Shao alisema hayo wakati wa mkutano wa wanachama wakupitia rasimu hiyo
ya katiba uliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Alisema kupita kwa rasimu
hiyo ni mwanzo mzuri hivyo ni wajibu wa kila mwanachama kuisoma na kuielewa
vizuri kwa ajili ya utekelezaji wa malengo ya mtandao huo.
Shao alisema baada ya rasimu
hiyo kukubalika kwa wanachama kilichobaki ni kwa wajumbe wa Kamati kuendelea
kusimamia zoezi zima la usajili,utakapokamilika mtandao uweze kuamza kazi
rasmi.
“Baada ya kukamilisha usajili
wa Katiba yetu wanachama wa
Tajonet watakutana Julai 19, mwaka huu kwa ajili ya kuangalia jinsi ya kukamilisha hatua muhimu ya uchaguzi wa kuwapata
viongozi watakaohudumu kwa kipindi cha miaka tatu”alisema Shao.
Aidha, mkutano huo ulipitisha
jina la Angela Msangi kuwa Mweka hazina ambapo kwa kauli moja wamekubaliana kuwa kila mwananachama
atawajibika kuchangia sh. I00,000
ikiwa ni ada ya uwananchama kila mwaka hata hivyo ada hiyo inaruhusiwa kulipwa
katika awamu mbili.
Shao aliwaasa wanachama
kuacha kuweka mbele chombo anakotoka na baadala yake kuamini kuwa kila
anachofanya ni kwa ajili ya maendeleo na famanikio ya TAJONE kitendo
kitakachokamilisha ndoto zao.
Kwa upande mwingine mtandao
huo umetoa shukurani kwa Meneja wa Hoteli ya Break point LT, Daud Machum kwa
kujitolea kwake ukumbi bure na sh 20,000 kama kuwaunga mkono katika kile
wanachokusudia.
Naye mweka hazina wa mtandao
huo, Angela alisema baada ya wanachama kutakiwa kuchangia mchango wa papo kwa papo kwa ajili ya kupata fedha
za huduma za kikao hicho, zilipatikana zaidi y ash 300,000 kutoka kwa
Wanchama 36 waliodhuria
mkutano huo.
No comments :
Post a Comment