Dalali Peter Hafumu akiongozwa na
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Wilson Mukama kwenye Mahakama hiyo akiwa
mnyonge na kuinamisha kichwa chini.
Wafuasi
wa Chama Cha CHADEMA wakiserebuka kwa furaha kwa kumbwaga chini Mbunge
huyo kwenye kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na Chadema, ambapo
hakimu wa Mahaka hiyo ya Igunga alikubali Hoja nane kati ya 13
zilizowasilishwa na Chadema.
KWA HUKUMU hiyo sasa, Jimbo la Igunga mkoani Tabora liko wazi kuanzia leo baada ya
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kumvua ubunge Peter Dalay Kafumu wa CCM kufuatia
hukumu iliyotolewa leo katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliomuweka
madarakani mbunge huyo ambayo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Kashindye.
Taarifa kutoka Tabora zimeeleza kuwa hukumu hiyo iliyovuta hisia za maelfu ya wakazi wa mji huo na maeneo ya jirani, ilisomwa kuanzia mishale ya saa 3:00 asubuhi. Pamoja na Kafumu, Kashindye pia aliwashitaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Protace Mgayane . Shauri hilo lilianza kusikilizwa na Jaji Mary Nsimbo Shangali tangu Machi 26, 2012. Akizungumza baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Kafumu amesema kuwa hajaridhishwa kwani yeye alichofanya wakati wote wa kampeni ilikuwa ni kunadi sera za chama chake (CCM). Kafumu aliongeza vile vile kuwa tangu awali, alishaeleza mara kadhaa kuwa haridhishwi na jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo kwa vile alikuwa akiegemea upande mmoja; na kwamba ndicho alichokifanya leo wakati akitoa hukumu. |
No comments :
Post a Comment