Katibu
mkuu wa wizara ya nishati na madini Eliakimu Maswi akiwa na Kaimu
kamishna mkuu wa wizara hiyo Ally Samaje na mwenyekiti wa Tamida hapa
nchini Sam Mollel wakiwa kwenye mkutano wa kujadiliana juu ya Bei
elekezi na ushirikiano jijini Arusha
*****
Mahmoud Ahmad Arusha
Wizara
ya nishati na Madini imesema kuwa haina tofauti na TAMIDA kwani chama
hicho kinatakiwa kutoa ushirkiano ili kuweza kuipeleka mbele sekta ya
madini kukuza na kuinua uchumi kupitia sekta hiyo.
Akizungumza
na wafanyabiashara wadogo wadogo wa vito jijini Arusha Katibu mkuu wa
wizara hiyo Eliakim Maswi alisema kuwa sekta hiyo ni muhimili wataifa
hivyo bei elekezi isiwe ndiyo ya kukwepa kuilipa mapato serekali na
kuwataka wanachama wa TAMIDA kushirikiana na serekali kuwafichua wezi
warasilimali zetu.
“Mtanzania
mzalendo ni Yule anayeilipa serekali kodi halali nanyi mnafanya hivyo
hivyo kuweni macho na wale wote wanaotaka kupandia mgongoni mwenu na
mtupe ushirikiano kuwafichua wale wote wanaohujumu sekta hii ya
madini”alisema Maswi.
Tamida
na wizara wamefikia makubaliano ya kutumia Bei elekezi hapa nchini ili
kutatua tatizo la bei linalowakumba wafanyabiashara wadogo hapa nchini
na kukuta wanauza bei ndogo kwa wajanja bila ya kuwa na taarifa ya bei
iliyoko sokoni kwa wakati huo.
Maswi
alisema kuwa zaidi ya usd.2.2 bilioni serkali ilikuwa inaidai kamuni ya
TANZANITE ONE kutokana na kodi ya tozo ya mrahaba waliyokuwa wamekwepa
kuilipa serekali tokea mwaka 2004
No comments :
Post a Comment