Baadhi ya miili ya wachimba migodi waliuawa na askari Afrika Kusini
Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza kipindi cha maombolezo nchini
humo kufuatia mauaji ya wachimba madini thelathini na wanne
yaliyofanywa na polisi,
wakati walipokuwa wakiandamana kudai malipo bora zaidi ya kazi.
Bwana
Zuma pia ametaka tume ya uchunguzi ya kisheria ichunguze mauaji hayo
katika mgodi wa madini meupe yaani PLATINUM eneo la Marikana.
Wakati huohuo wachimba madini wameamriwa kurejea kazini siku ya Jumatatu la sivyo watafukuzwa kazi.
Lakini wengi wamesema kumaliza mgomo wao sasa ni sawa na kuwadhalilisha wenzao waliouawa.
Wanasema watarejea kugoma katika eneo la mgodi huo na wataendelea kushinikiza malipo bora zaidi ya kazi.
Hata
hivyo chama cha wafanyakazi wa migodi cha NUM ambacho kina uhusiano wa
karibu na chama tawala cha ANC - kinasema wanachama wake wamekubali
kurejea kazini.
Mmoja wa
wachimba madini hao Vuyisile Mchiza, amesema atarejea kazini iwapo
idadi kubwa ya wenzake watakubaliana kusitisha mgomo.
''Iwapo
idadi kubwa watarejea kazini kesho, basi na mimi nitakwenda''. Anasema.
''Iwapo wengi hawatakwenda kazini, nami pia sitakwenda, kwasababu
sitaweza kufanya kazi wakati wengine wakiwa bado wanaomboleza''.
Ameongeza.
No comments :
Post a Comment