LAGOS, Nigeria
KUFUATIA Nigeria kuvurunda na kurudi bila hata medali moja ya mashindano ya Olimpiki 2012 jijini London,
rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan ameagiza mageuzi na mabadiliko
makubwa na ya haraka katika tasnia ya michezo, kupitia wizara husika.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari wa Nigeria, Labaran Maku, wakati wa
mkutano wake na vyombo vya habari uliofanyika Ikulu ya nchi hiyo, baada
ya kikao cha kila wiki cha Rais na Baraza Kuu la Utendaji (FEC)
Jumatano.
Waziri Maku alisisitiza kuwa, rais
amesikitishwa kwa kilichofanywa na wawakilishi wa nchi hiyo jijini
London, na kwamba ametaka kuwapo kwa haja ya kubadili mwenendo huo
mbovu.
Kwa mujibu wa waziri Maku, rais
Jonathan, ameagiza kuwapo kwa utaratibu wa wizara na vyama vya michezo
kushirikisha serikali za majimbo, sekta binafsi na wadau wengine, ili
kuweka kipaumbele cha mafanikio ya michezo nchini humo.
"Yeye
(rais Jonathan) amesema kufanya kwetui vibaya jijini London,
kuchukuliwe kama changamoto ya ya harakati mpya za kuirejeshea heshima
michezo ya nchi hiyo ambayo, imeanza kupotea kutokana na lindi la
kuvurundano kwenye mashindano makubwa.
"Rais
Jonathan anaamini kwamba ili kubadili mazingira na hali ya sasa ya
kufanya vibaya, tunahitaji wataalamu, tunahitaji mipango yakinifu na
tunahitaji kufadhili michezo katika mfumo utakaowezesha nchi kurejesha
mvuto na maendeleo katika sekta hiyo.
"Yeye
anaamini kwamba katika mashindano yajayo ya Jumuiya ya Madola na
Olimpiki ijayo ya mwaka 2016 nchini Brazil, lazima Nigeria kama taifa
lilenge kutimiza malengo binafsi kayika ukuzaji wa michezo ili
kuimarisha ushiriki wa wawakalishi," alisisitiza Waziri Maku.
No comments :
Post a Comment