Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
* Adai wana njama za kuuza nchi kwa mataifa tajiri
*Awataka wataje mabilioni wanayopewa nje na mikataba yake.
* Asema harambee zao ni changa la macho
* Ahofia tamaa ya mataifa makubwa kwa rasilimali za nchi masikini
Na Mwandishi Wetu, Jijini Dar
CCM
imesema imesikitishwa na iliouita usanii mkubwa unaofanywa na Chadema,
kuwahadaa Watanzania kwa kufanya harambee kwa lengo la kuhalalisha
mabilioni ya chama hicho yanayodaiwa kutolewa na wafadhali kutoka
mataifa tajiri duniani.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
aliyasema hayo leo, Agosti 12, 2012, wakati akizungumza na waandishi
wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba
jijijni Dar es salaam.
“Itakumbukwa
mara kadhaa Chadema wamekuwa wakiitisha harambee za kisanii kwa
kujaribu kuwahadaa baadhi ya Watanzania kwa kuwaomba wakichangie chama
hicho huku viongozi wa chama hicho wakijua kuwa tayari wameshapata
mabilioni toka kwa wafadhili wao. Mfano mzuri wa usanii huu ni juzi
siku ya Jumamosi, Agosti 10, 2012, kwenye hoteli ya Serena ambapo
walifanyika kiini macho cha harambee na kurushwa moja kwa moja na kituo
kimoja cha televisheni." alisema Nape.
Alisema
,umekuwa ni utamaduni wa Chadema kuhadaa watu kwa kuitisha harambee za
kisanii kina wanapokuwa wameshapewa mabilioni ya fedha na wafadhili wao,
ili mradi wahalalishe kuwa fedha wanazotumia zimetokana na michango ya
watanzania wakati si kweli.
Nape
alisisitiza kuwa CCM wanao ushahidi kuhusu zinakotoka fedha na
mikataba wanayoingia Chadema na wafadhili hao na kudai kuwa kama
hawatasema wenyewe basi yeye (Nape) ipo siku atawasaidia kwa kutaja
wafadhili hao na kuanika hadarani mikataba hiyo.
“Tunao
ushahidi wa kutosha unaoonyesha mabilioni waliyopewa Chadema juzi na
wafadhili kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuendeleza operesheni zao
mbalimbali nchini. Cha kushangaza badala ya kuwaambia wanachama wao na
Watanzania kwa jumla mikataba na wanakoyapata mabilioni haya,
wanawahadaa kwa kuwachangisha na kugeuza mapato hayo mtaji wa baadhi ya
watu binafsi ndani ya chama”, Alisema Nape
Nape
alidai kwamba, siri kubwa inayofichwa kuhusu mikataba na mabilioni
wanayopewa Chadema ni kwa sababu wanaotoa fedha hizo wana ajenda ya
kunyemelea rasilimali za nchi hii zinazoanza kuonyesha matumaini ya
kuwepo kwa wingi ili wapate kizikwapua kwa urahisi kupitia mgongo wa
chama hicho.
"Kwanini
mabilioni hayo yanatolewa kwa Chadema wakati huu ambapo sasa Tanzania
imo katika kufanya utafiti na ugunduzi wa rasilimali mbalimbali zikiwamo
gesi na mafuta? Na Je ufadhili huu kwa Chadema licha ya kufichwa sana
na kufanywa siri, una nia njema kwa nchi yetu na rasilimali za nchi
yetu? Kwanini ufadhili huu wa mabilioni unafanywa siri ya watu wachache
hata ndani ya chama chenyewe?", Nape alihoji.
Alisema,
hatua hiyo ya Chadema itaitumbukiza Tanzania katika machafuko
yasiyoisha, kama ambavyo inashuhudiwa katika baadhi ya nchi zenye
rasilimali kama madini ambako nchi zenye utajiri wa fedha zilijipenyeza
kupitia walioitwa wapambanaji wa uhuru na haki katika nchi hizo na hadi
sasa hakuna amani.
"Migogoro
mingi tunayoshuhudia hasa katika nchi zinazoendelea pamoja na kuwepo
sababu zingine lakini moja ya chanzo kikubwa ni uwepo wa utajiri wa
rasilimali mbalimbali ambapo mataifa makubwa huzitamani na njia pekee ya
kuzipata kwa urahisi ni kuchochea migogoro ya ndani na hivyo kuwa
rahisi kupora rasilimali hizo wakati wenye nchi wanahangaika katika
migogoro na kuachwa wakiwa masikini wa kutupwa huku waadhirika wakubwa
wa migogoro na vita hivi vikiwanufaisha wakubwa.” Alisema Nape.
Nape
alitoa mwito kwa Watanzania kuwa ni muhimu macho na ulaghai huo wa
Chadema na wafadhili wao na kukitaka chama hicho na wafadhili wao kama
kweli wana nia njema na Tanzania, waweke wazi mashariti ya ufadhili huo
wa mabilioni ya fedha ili Watanzania wote wajue kama yana manufaa kwao
au la hasa ikizingatiwa kuwa vyama vya siasa hapa nchini vinaendeshwa
kwa fedha za walipa kodi, hivyo Watanzania wana haki ya kujua.
Pamoja
na kuwataka kuweka wazi mashariti yanayoambatana na mabilioni hayo Nape
aliwataka Chadema waseme hadharani wenyewe kwamba wamepewa mabilioni
hayo, na kuwataka waache mara moja kuwahadaa Watanzania na kujaribu
kujipachika kuwa ni Chama cha wanyonge kinachotegemea kujiendesha kwa
michango ya watanzania huku wakiendelea kuchukua mabilioni kwa siri
kutoka nje.
“
Wasipowaeleza watanzania ukweli , tutawasidia kuwaeleza watanzania
ukweli wa kiasi halisi cha mabilioni haya, walikozitoa na mikataba
waliyoingia. Lengo la hili ni kuhakikisha kuwa nchi yetu haiwekwi rehani
kwa uroho wa madaraka wa baadhi ya wana siasa.” Nape alisema.
Nape
akawaasa wanasiasa, kuendesha siasa za nchi kwa kuzingatia uzalendo na
kukwepa kudumbukia kwenye tamaa za madaraka kujisahau na kuwa tayari
hata kuweka nchi rehani, hasa kipindi hichi ambapo ugunduzi wa
rasilimali mbali mbali hasa madini, gesi na mafuta vikiwa vinashika kasi
nchini na kwamba ugunduzi huo uwe baraka kwa nchi badala ya laana na
kuwa chanzo cha kuiuza nchi.
No comments :
Post a Comment