Na Andrew Chale
MWANAMITINDO maarufu nchini, Ally Rehmtullah pichani juu atazindua onyesho rasmi la kazi zake mpya za
mitindo ya mavazi mbalimbali kwa wanawake na wanaume ‘Ally Rehmtullah
2013 Collection’lililopangwa kufanyika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, Septemba 8 2012.
Rehmtullah
alisema dhumuni la kuandaa onyesho hilo la kipekee ni kuweza kuonyesha
aina mpya ya mitindo ya mavazi aliyobuni hivi karibuni na harakati za
kuinua kiwango cha kazi za mitindo kwa Tanzania.
“Nimepania kupanua wigo wa taaluma ya mitindo na mavazi hapa nchini, ili
kazi za wanamtindo na wabunifu ziweze kupenya kwenye soko la ndani na
la Afrika Mashariki na ya kati wakati tayari kuna soko la pamoja katika
jumuiya ya Afrika mashariki,’ alisema.
Pia
aliongeza kuwa, kwenye uzinduzi huo mavazi na onyesho litapambwa kwa
rangi nyeupe, ubunifu wa hali ya juu pamoja na muonekano mpya wa mavazi
yaliyofanyiwa utafiti mkubwa ili kuweza kuendana na utamaduni wa
mwafrika.
Aidha,
Rehmtullah alisema licha ya kuonesha mavazi pia kutakua na burudani
mbalimbali kutoka kwa wasanii nyota, ambapo pia aliwataja wadhamini
wakuu wa onyesho hilo kuwa, Mercedez Benz, Mo Blog, Belvedere Vodka,
Dulux, Raha, Hugo Domingo,The Tanzanite Experience, Shiva Images, Farm
Plant, Creative Infinities, Out Door, Stanbic Bank, Phoenicia
Properties, Dar es Salaam Serena Hotel, Missie Popular Blog, Quality
Furniture na Mx Carter.
Katika onesho hilo, linatarajia kudhuriwa na watu 400, wakiwemo viongozi wa serikali, wafanyabiashara na wageni mbalimbali ambapo watashuhudia wanamitindo wengine mahili na chipukizi watakaoonesha mitindo siku hiyo.
No comments :
Post a Comment