Askari Polisi wakiwa katika doria kufuatia vurugu kubwa zilizotokea katika eneo la Kariakoo
Askari Polisi akijiandaa kurusha mabomu ya machozi ili kukabiliana na vijana waliokuwa wakirusha mawe.
Moja, mbili, tatu
Askari Polisi akiweka mabomu ya machozi katika bunduki yake huku akiangalia hali ya usalama wake.
Mmoja wa vijana waliokamatwa katika eneo hilo
Askari
Polisi wakimdhibiti mmoja wa vijana waliokamatwa katika vurugu
zilizotokea katika mtaa wa Kongo na Mchikichi jijini Dar es Salaam jana
kufuatia mgogoro wa kugombea nyumba namba 86 inayomilikiwa na Samiri
Said
Majerui katika vurugu hizo
Baadhi ya vijana waliokamatwa katika vurugu hizo wakiwa katika gari la Polisi lenye namba za usajili T 220 AMV
Kijana aliyekaidi amri ya Polisi wakati akipita katika eneo lililokuwa na vurugu akiwa chini ya ulinzi
Mmiliki halali wa nyumba hiyo, Samiri Said
Nyumba inayolalamikiwa ikianza kuvunjwa
Mtaa wa Kongo ukiwa hauna mweupe
Mtaa wa Mchikichini Kariakoo ukiwa hauna watu kutokana na vurugu zilizotokea leo
Mtaa wa Mkunguni ambao huwa na pilikapilika nyingi ukiwa mtupu kufuatia wafanyabiashara kufunga biashara zao
Nyumba inayolalamikiwa inayogombewa na pande mbili.
DAR ES SALAM, Tanzania
RISASI
na mabomu ya kutoa machozi leo vilirindima katika maeneo ya Kariakoo
baada ya mtu mmoja kuvamia nyumba kwa zaidi ya miaka 40 akidai kuwa ni
yake.
Hali
hiyo imekuja baada mmiliki halali wa nyumba hiyo, Samiri Said kushinda
kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo mahakama ili mtaka mtu
huyo aliyetambulika kwa jina la Shaban Hassan kuondoka katika nyumba
hiyo.
Akizungumza
katika eneo la tukio kiongozi wa Kampuni ya Udalali ya Yono, Isaac
Nguku alisema walifika eneo hilo kwa amri ya Mahakama kwa lengo la
kukabidhi nyumba hiyo kwa Said.
Amesema
kuwa hata hivyo, walipofika katika eneo hilo majira ya saa 5:00 asubuhi
walikuta kundi la vijana ambao inasadikika kuwa waliandaliwa na Hassan
kwa ajili ya kukwamisha zoezi hilo.
Nguku alisema baada ya kuona hali hiyo waliamua kuomba msaada kutoka polisi ambapo walifika na kuanza kuwatawanya vijana hao.
“Vijana
hao hawakuridhika ndipo wakaanza kuturushia mawe kutoka kila
kona walizokuwa wamejipanga kitendo hicho kilisababisha askari kufyatua
risasi za moto juu huku wakipiga mabomu ya machozi na kuwatawanya mbali”
alisema Nguku.
Baada
ya vijana hao kutawanyika mitaa minne inayozunguka nyumba hiyo
ilifungwa, mitaa hiyo ni pamoja na Kongo, Mkunguni, Tandamti na
Mchikichini
Naye
mmiliki wa nyumba hiyo, Said alisema wavamizi hao walipanga katika
nyumbani hiyo tangu mwaka 1972 ambapo baada ya hapo wakajitengezea hati
bandia kwa lengo la kumdhulumu mama yake mzazi.
Alisema
kitendo hicho kiliwafanya wafikishe kesi hiyo mahakamani ambako
waliwakilisha hati zao ambazo zimewafanya washinde kesi hiyo, mvamizi
huyo kuamriwa aondoke kitendo alichokipinga huku akikata rufaa za mara kwa mara lakini hata hivyo akawa anashindwa mara zote.
No comments :
Post a Comment