Mwenyekiti
wa Kia motors, Cho
Kwi Hyun akimkabidhi MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik mfano
wa ufunguo wa moja ya magari manne ambayo kampuni hiyo imetoa kwa shule
ya Maendeleo iliyopo Nakasangwe Madale wakati wa hafla ya uzinduzi wa
shule hiyo leo kulia ni Mkurugenzi Shirika (GNI), Yang Jin OK na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali Mtaa Madale Alex Mbuya
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam Said Meck Sadik akihutubia wananchi wakati wa uzinduzi
wa shule ya Maendeleo iliyoko Nakasangwe Madale jijini Dar es salaam
iliyojengwa kwa msaada wa kampuni ya KIA na HYUNDAI za Korea kupitia
shirika la Good Neighbor International la Korea
Vijana
mbalimbali kutoka Shirika la GNI nchini Korea walioshiriki kujitolea
kujenga shule ya Sekondari Maendeleo Nakasangwe huko Madale wakiwa
katika hafla ya uzinduzi leo.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaaam Said
Mecky Sadik ameitaka Manispaa Kinondoni inahakikisha kuwa wanakamilisha ujenzi
wa vyumba vya madarasa 249 kwa ajili ya watotoa watakaofaulu kuingia kidato cha
kwanza mwaka ujao.
Kauli hiyo aliitoa leo, wakati wa
uzinduzi wa shule ya sekondari Maendeleo, iliyojengwa kwa msaada wa Shirika la
Good Neighbor (GNI), kwa kushirikiana na Kia Motors kutoka Jamhuri ya Korea.
Sadik alisema ujenzi wa vyumba hivyo utasaidia
kuwafanya watoto zaidi 18000 wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza katika
wilaya hiyo kuanza masomo kwa wakati.
Aliwataka viongozi wa Wilaya hiyo,
kutekeleza kwa vitendo ahadi waliyotoa kuwa ifikapo mwishoni mwa Desemba mwaka huu watakuwa mmekamilisha ujenzi
wa vyumba hivyo.
Akizungumzia kuhusu shule hiyo, Sadik
alisema ujenzi wa shule hiyo utasaidia katika kuwapatia watoto elimu bora.
“Mmepata msaada huu lakini ni
washauri kuwa unapobebwa ni lazima ujikaze hivyo msibweteke bali mhakikishe
mnazilinda mali za shule hii kwa nguvu zenu zote”alisema Sadik.
Vilevile alisema uwezekano wa mtaa
huo kupatiwa nishati ya umeme inawezekana, lakini bado wakazi wa maeneo waache
kujenga bila kufuata taratibu za mipango miji kwa ajili ya huduma za jamii.
Naye Mwenyekiti wa Kia motors, Cho
Kwi Hyun alisema ukiachilia mbali ya ujenzi wa shule hiyo, pia wamekabidhi
magari manne yatakayotumika kusafirisha wanafunzi na huduma nyingine za kijamii
katika mtaa huo.
Kwa Upande Mkurugenzi Shirika (GNI), Yang Jin OK
alisema mradi huo utakuwa wa miaka mitano hivyo anawaomba wananchi kutoa
ushirikiano kwa ajili ya kujisogezea
No comments :
Post a Comment