Beki
wa kimataifa wa timu ya Yanga ya Dar es Salaam, Mbuyu Twite,
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana wakati
alipowasili akitokea Rwanda, tayari kwa kujiunga na timu yake ya Yanga
baada ya gumzo la muda mrefu na mvutano wa hapa na pale wa Watani wa
Jadi Yanga na Simba, ambao kila mmoja alikuwa kijinadi kuwa amemsajili
mchezaji huyo huku mmoja akibaki kuambulia manyoya.
Akizungumza
na mtandao huu kuhusu kutua nchini huku akiwa ametinga Jezi no 4, yenye
jina la Mwenyekiti wa Simba Ismail Rage, beki huyo amesema kuwa yeye ni
mchezaji kama walivyo wengine na anatambua kuwa ametua katika timu
yenye upinzani mkubwa na mahasimu wao Simba, hivyo yeye ametua
kuendeleza Utaji wa Jadi baina ya timu hizo, na ndiyo maana ameamua
kuvaa jezi yenye jina la Rage, ili kuonyesha maana halisi ya utani huo
pamoja na kutokea mtafaruku wa hapa na pale kati ya vilabu hivyo.
Aidha
Twite, amesema kuwa ''Namuheshimu sana Rage, na namuomba aniache
nifanye kazi niliyotumwa na Baba yangu kama alivyoniamini na kuniruhusu
kuja kuitumikia Yanga na kuwarejeshea Faranga yao Simba'' alisema Twite
kwa kiswahili kilichopindapinda.
Twite
amewataka mashabiki wa Yanga kumuamini na kupuuza yanayoendelea kuenea
juu yake kuwa huenda akikosa kuichezea timu hiyo kutokana na kuchanganya
madawa na kusema kuwa yeye ni mchezaji halali wa Yanga timu ambayo
imefuata taratibu zote zinazotakiwa.
''Ujue
hata mimi nilikuwa na wasiwasi japo nilipokea faranga za Rage, kwani
hatukufanya vile imefanya Yanga hadi kufikia jana nilipopokelewa na
mashabiki wengi wengi wengi sana wa yanga pale kwa uwanja wa Ndege''
alisema Twite.
Mbuyu Twite, akilakiwa na mashabiki lukuki wa Yanga kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana.
No comments :
Post a Comment