Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, August 10, 2012

Maandalizi ya mashindano ya Kimataifa ya kuhifadhi na kusoma Qur'an Tukufu yakamilika



Mratibu wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa, Sheikh Othman Kaporo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya mashindano hayo, yatakayofanyika kesho na keshokutwa katika ukumbi wa Starlight na Diamond Jubilee jijini. Katikati ni mmoja wa majaji wa mashindano hayo, Dk. Abbas Hamza kutoka Sudani na mshiriki kutoka Yemen, Fawaz Ahmed. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

 Mmoja wa washiriki wa mashindano ya Kimataifa ya kuhifadhi na kusoma Qur'an, kutoka Phillipines, akisoma baadhi ya Aya za Qur'an Tukufu wakati wa mkutano huo leo. 

 Mshiriki wa mashindano ya Kimataifa ya kuhifadhi na kusoma Qur'an, kutoka Misri, ambaye ni mlemavu wa macho (kipofu), akisoma baadhi ya Aya za Qur'an Tukufu wakati wa mkutano huo jijini leo. 

 Mshiriki wa mashindano ya Kimataifa ya kuhifadhi na kusoma Qur'an, kutoka China, Suleiman (9), aliyehifadhi Juzuu 30 (msaafu mzima), akisoma baadhi ya Aya za Qur'an Tukufu wakati wa mkutano huo jijini leo. 

 Mmoja wa Majaji wa mashindano hayo, Dk. Abbas Hamza kutoka Sudani, akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Mratibu wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa, Sheikh Othman Kaporo.

 Mratibu wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa, Sheikh Othman Kaporo, akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano huo Dar es Salaam leo. Kulia ni mmoja wa majaji wa mashindano hayo, Dk. Abbas Hamza kutoka Sudani na kushoto ni mshiriki kutoka Nigeria, Ustaadh Muhammad Abdallah.
Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi na kusoma Qur'an Tukufu ya Kimataifa, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya mashindano hayo, yatakayofanyika kesho na keshokutwa katika ukumbi wa Starlight na Diamond Jubilee jijini.

No comments :

Post a Comment