Mshambuliaji Mtanzania Mbwana Samata wa TP Mazembe ya Congo-DRC (kulia) akiwajibika dimbani katika moja ya mechi za klabu hiyo.
CAIRO, Misri
Katika
mechi ya awali iliyopigwa Agosti 4 huko Stade TP Mazembe jijini
Lubumbashi, Mazembe iliichapa Zamalek, shukrani kwa mabao ya Ngandu
Kasongo dakika ya 70 na Mbwana Samata dakka ya 77
WASHAMBULIAJI Tresor Mputu na Mbwana Samata
waliofunga mabao 10 kati ya 16 iliyofunga TP Mazembe hadi sasa katika
Ligi ya Mabingwa Afrika, kesho watakuwa katika jaribio la kuizamisha
Zamalek nyumbani katika mechi ya nne hatua ya makundi.
Mputu na Samata, wamebeba matumaini ya
Mazembe kuiduwaza Zamalek ya Misri ambao ni mabingwa wa zamani Afrika
wanaonolewa na kocha Jorvan Vieira, pambano litakalopigwa kwenye Uwanja
wa Jeshi jijini Cairo.
Mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Slim
Jedidi wa Tunisia, itatumiwa na Mafarao hao kulipa kisasi cha kuchapwa
mabao 2-0 mapema mwezi huu, huku ikipanga kutumia kisasi hicho
kuitibulia Mazembe inayosaka pointi muhimu.
Kutokana na msimamo wa kundi B ulivyo,
Zamalek haiwezi kubadili nafasi yake mkiani mwa kundi bila pointi,
ingawa inaweza kuiharibia Mazembe iliyo na pointi nne kwenye nafasi ya
pili, kama ilizonazo Berekum Chelsea inayoingia dimbani kuivaa Al Ahly
kesho.
Al Ahly
inaongoza kundi ikiwa na pointi tisa na kama itamudu kuichapa Berekum
itajihakikishia nafasi ya kutinga nusu fainali, ambayo Mazembe
inapigania ushindi wa angalau mechi mbili kati ya tatu za raundi ya pili
kufuzu hatua hiyo.
Mapema juzi, Vieira Mbrazil anayeinoa
Zamalek, alitangaza wakali 20 watakaobeba jukumu la kupigania heshima ya
klabu hiyo dhidi ya Wakongo hao, ambapo alimtema kikosini winga
Mohammed Abd Al Shafi na kumrudisha kiungo Ahmed aliyekwaruzana na
kutemwa na kocha aliyepita Hassan Shehata.
Katika mechi ya awali iliyopigwa Agosti 4
huko Stade TP Mazembe jijini Lubumbashi, mabao mawili yaliyofungwa na
Ngandu Kasongo dakika ya 70 na Mtanzania Samata dakka ya 77, yaliipa
ushindi muhimu baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Berekum ya Ghana.
Kama itakubali kichapo katika mechi ya
kesho, Zamalek itakuwa imepoteza rasmi nafasi ya kufuzu nusu fainali,
ikiwa na mechi mbili mkononi, ambapo nyota wa Berekum Chelsea, Emmanuel
Clottey anaongoza mbio za Kiatu cha Dhahabu akiwa na mabao 12.
No comments :
Post a Comment