KINSHASA, DRC
KIONGOZI
na mmiliki wa bendi ya Quartier Latin ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC), Koffi Charles Antoine Mumba Olomide, jana alipandishwa
kizimabi juzi jijini Kinshasa, akishitakiwa kwa kupigana mtayarishaji
(Producer) wake Diego Lubaki.
Habari kutoka
jijini humo zinasema ya kuwa, Olomide, mwanamuziki mashuhuri barani
Afrika, ameshitakiwa kwa kumpiga mtayarishaji wake huyo wa siku nyingi,
kutokana na madai ya kudaiana pesa kiasi cha dola za Kimarekani 3,680.
Olomide,
56, alikamatwa na kufikishwa kituo kimoja cha polisi, kabla ya
kufikishwa mahakani juzi Jumatano, kabla ya kutakiwa kurejeshwa hapo
jana Alhamisi ili kutajwa rasmi kwa kesi hiyo.
Taarifa zinapasha kuwa, tangu wakati wa mzozo, kukamatwa, kufikisha
kituo cha polisi na hatimaye mahakamani, tukio hilo lilivuta hisia za
wengi miongoni mwa mashabiki wa mkali huyo na muziki wa Kikongo kwa
ujumla.
Olomide
aliyetamba na vibao kadhaa kikiwamo cha Force de Frappe ‘Nguvu ya
Kupiga,’ alidokezwa mahakamani hapo na hakimu kuwa, iwapo atapatikana na
na hatia katika kesi anayotetewa na mawaikili 10, anaweza kufungwa jela
miezi sita.
Koffi Olomide mkali mwenye
mafanikio makubwa kwenye tasnia ya muziki DRC, uliompa tuzo kadhaa za
Kora, ikiwamo ya mwaka 2002 iliyokuja baada ya ile ya Msanii Bora wa
Afrika wa mwaka 1998.
Mafanikio yake katika muziki wa Soukouss, elimu kubwa akiwa na Shahada
ya Uchumi na Biashara, ni kati ya vitu vilivyoweka jina lake juu
miongoni mwa wasanii barani Afrika – ingawa amekuwa akiishi ya nchi yake
miaka mingi sasa.
No comments :
Post a Comment