Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, August 14, 2012

Balozi wa Tanzania Uingereza,Peter Kallaghe Awapongeza na Kuwaaga Wawakilishi Wetu Walioiwakilisha Nchi Kwenye Mashindano Ya Olimpiki Nchini Uingereza



 Toka kushoto, Kocha Remmy Ngabo(ngumi), Kanali  Pellegreen Mrope (Afisa Ulinzi, Ubalozini), Kocha Zachariah Gwandu (riadha) na Amos Msanjila(Afisa Mambo ya Nje Ubalozini, Daraja la Pili ).
 Mwanahabari Frank Eyembe wa Urban Pulse (katikati) akiwa na kocha wa kuogelea, Sheha Mohammed Ali na kocha wa masumbwi, Remmy Ngabo katika tafrija ndogo kuwaaga wanamichezo wetu London.
 Balozi wetu Peter Kallaghe akiwa na wahudumu wa Olimpiki wasiolipwa mshahara, Lesley Shayler, Alison Cochrane na Steve Wiseall. Wa kwanza kulia ni Balozi wa Rwanda, Uingereza Mheshimiwa  Ernest Rwamucyo.
 Balozi wa Tanzania Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe( wa nne aliyesimama nyuma toka kulia) akiwa na wanamichezo, makocha, maofisa na wahudumu wa kujitolea Olimpiki. Kulia kwake ni mkuu wa msafara, Bwana Hassan Jarufu na Balozi wa Rwanda, Mheshimiwa Ernest Rwamucyo (wa kwanza kulia) nyumbani kwake alipowaalika kuwapongeza na kuwaaga jana Jumatatu.Picha Zote na Freddy Macha
--
Balozi wa Tanzania Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe amewapongeza wanamichezo wetu walioiwakilisha nchi katika Olimpiki kwa nidhamu na kuwataka wasivunjike moyo kwani sio sisi tu tuliokosa medali.
“Wanamichezo wetu wameonyesha tabia bora kinyume na watu wa nchi nyingine waliofanya mambo ya aibu sana. Lazima tuwapongeze kwa kufikia viwango na kuibeba bendera ya Tanzania,”alisema.
Akiongea katika tafrija ndogo kuwaaga wanamichezo saba, maofisa na makocha wao, Balozi Kallaghe alisisitiza kwamba  tusiwalaumu wanamichezo kwa kushindwa kwani kuna mataifa mengi yaliyokosa medali. Tafrija hiyo ilihudhuhuriwa na maofisa wote wa Ubalozi, wanahabari London na Balozi wa Rwanda Uingereza, mheshimiwa Ernest Rwamucyo.
Kitakwimu ni asili mia kumi tu ya washiriki 10,500 waliocheza michezo 26 (toka mataifa 204) wakapata medali. 
“Kuna mataifa tajiri kama Ujerumani, Australia na India ambayo hayakufanya vizuri na pia wenzetu Afrika mfano Kenya na Ethiopia ambao hawakuridhika au kufikia nafasi waliyozoea miaka iliyopita.”
Balozi aliitaja nchi ya Wafilipino (Philippines) yenye watu Millioni 93 ambayo ilikuwa na wachezaji 11 na haikuambulia kitu.  Kidesturi toka 1936, Wafilipino wamekuwa wakishinda medali katika mchezo wa ngumi.
“Lazima tujiulize maswali ili kufanikiwa mashindano yajayo na kujitayarisha ndiyo msingi. Vipaji vingi vipo Tanzania. Tujaribu  kuangalia na kujiuliza wapi vilipo vianzio vya kuendeleza michezo yetu kutoka ngazi za chini maana uwezo wa kushinda tunao. ”
Akipigiwa makofi balozi alimtaja mkimbiaji maarufu wa Uingereza mwenye asili ya Kisomali, Mohammed “Mo” Farah aliyefanya vibaya sana Olimpiki ya 2008, China. “Baada ya kushindwa kabisa Beijing, Mo Farah alijilaumu na kulia sana; ila hakuvunjika moyo; alirudi akajiandaa vizuri na matokeo yake mwaka huu kashinda medali mbili za dhahabu.”
Naye mkuu wa msafara  Bwana Hassan Jarufu aliushukuru ubalozi wetu Uingereza kwa ukaribisho mzuri uliohakikisha kwamba wanamichezo wako sawa toka walipowasili hapa majuma mawili kabla ya Olimpiki.  Aliwataja pia wasaidizi wenyeji wa Uingereza, Alison Cochrane, Steve Wiseall na Lesley Shayler aliyewahi kuitembelea Bongo na kuipenda sana.
 “Hawa wamekuwa wenyeji wetu wazuri sana,” alisema.
Bwana Jarufu alifahamisha kwamba wanamichezo wetu shurti kupongezwa kwa kujitahidi kufanya shughuli hii bila ajira au kazi maalum.
“Kwa mfano wakimbiaji wa mbio za marathon wanatakiwa kiafya wakimbie mara nne tu kwa mwaka kusudi wawe tayari kwa mashindano makubwa, lakini kutokana na kukosa ajira au msaada wa kifedha wanalazimika kushindana mara nyingi zaidi ili waishi. Na si ajabu ukamsikia mmoja mmoja akilalamika kashindwa mashindano makubwa kama Olimpiki kutokana na majeruhi fulani mwilini.”
Katika michuano ya siku ya mwisho Jumapili wanariadha watatu, Faustin Mussa, Samson Ramadhan na Mohammed Msondiki Ikoki walishiriki mbio za marathon na hawakupata medali yeyote.  Mshindi alitoka Uganda Stephen Kiprotich akifuatiwa na Wakenya: Abel Kirui na Wilson Kiprotich.
Habari zaidi tembelea :www.kitoto.wordpress.com

No comments :

Post a Comment