Mafundi
wa ujenzi wa Barabara wakiendelea na kazi ya uchimbaji eneo la katikati
ya barabara za jijini Dar es Salaam, ili kujenga Njia ya Mabasi
yaendayo kasi, Hapa ikiwa ni eneo la Mkwajuni Kionondoni, ambapo mawazo
ya walio wengi ni kuwa baada ya kukamilika kwa mradi huo wa ujenzi wa
njia hizo na kuanza kazi kwa mabasi yaendato kasi basi huenda foleni
zikawa ndiyo kikomo kama si kupungua. Je nini mawazo yako Mdau juu ya
hili mradi hu utakapokamilika Foleni zitapungua ama zitaongezeka?
Eneo
la Bonde la Mkwajuni Kinondoni, ambalo tayari eneo hili la katikati ya
barabara lilikuwa limeachwa 'jembamba' sasa wataalam wanatarajia
kutushangaza kwa lipi katika eneo hili, ili kupitisha njia hii ya mabasi
yaendayo kasi?
Hapa
ni eneo la Bonde la Kawe, Barabara ya Bagamoyo, mafundi wakiendelea na
zoezi la kupachika daraja katika eneo hili la barabara hiyo mpya, je
kukamilika kwa barabara hii, kutasaidia kupunguza foleni ama kutaongeza
foleni kwa kufanya hata wale wenye majumba yao ya kifahari ambao
walijenga na kuamua kuhamia mjini na kuyaacha majumba yao na kupangisha
ili kukwepa foleni na wao pia wote si watareja na hivyo kuongeza tena
msongamano?
Hapa ni eneo la Lugalo, ukitokea Mwenge, mafundi wakiwa katika harakati za kujenga daraja jipya na kubomoa lile la zamani.
Hapa ni eneo la Kimara Barabara ya Morogoro, mafundi wakiendelea na zoezi la ujenzi wa Njia ya Mabasi yaendayo kasi.
Hii ni sehemu tu ya foleni za asubuhi ya jijini Dar es Salaam, hapa ni
Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, eneo la Oysterbay Polisi kabla ya taa za
kuongozea magari za Namanga, leo asubuhi.
Je
ipo siku Jiji hili la Dar es Salaam, litakuja kuwa kama hivi barabara
nyeupeeeee, baada ya kukamilika mradi huo ama itakuwa ni ndoto?? zaidi tembelea http://sufianimafoto.blogspot.com/
No comments :
Post a Comment