TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama Cha Mapinduzi kimetafakari hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyotolewa jana Agosti 21, 2012 na Mahakama Kuu kanda ya Tabora.
Kimejiridhisha
na kufanya uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya uchaguzi,
dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga mkoani Tabora Dokta Dalaly Peter
Kafumu.
Kusudio hilo linatokana na kutorishwa na hukumu hiyo.
Imetolewa na;-
Nape Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM WA
ITIKADI NA UENEZI
22/08/2012
*******************************************
*******************************************
NA MWANDISHI WETU
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakikuridhishwa na hukumu iliyotolewa na
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga, Peter
Dalally Kafumu.
Taarifa
iliyolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi,
Nape Nnauye mchana leo, imeseme kufuatia kutoridhishwa na hukumu
iliyotolewa jana na Jaji wa Mahakama hiyo, Mary Shangali, kitakata
rufani.
"Chama
Cha Mapinduzi kimetafakari hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyotolewa jana
Agosti 21, 2012 na Mahakama Kuu kanda ya Tabora. Kimejiridhisha na
kufanya uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya uchaguzi,
dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga mkoani Tabora Dokta Dalaly Peter
Kafumu.Kusudio hilo linatokana na kutorishwa na hukumu hiyo". imesema
taarifa hiyo.
Jana
Jaji Mary Shangali katika hukumu yake, alisema ametengua ushindi wa
Dk. Kafumu baada ya kurishishwa na madai saba kati ya 17
yaliyowasilishwa katika mahakama hiyo na Mlalamilikaji, aliyekuwa
mgombea kwa tiketi ya Chadema, Joseph Kashindye.
Dk.
Kafumu wa CCM alitangazwa kushinda kiti na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo
la Igunga, katika uchaguzi mdogo uliofanyika, Septemba mwaka jana, baada
ya kujiuzulu aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Rostam
Aziz.
No comments :
Post a Comment