Ni Matonya aliyepata umaarufu zaidi baada ya mkuu wa zamani wa mkoa wa Dar es salaam, Yusuf Makamba kumtimua jijini na kuagiza mamlaka husika kuhakikisha haruhusiwi kuingia kwenye mipaka ya Dar es salaam.
Ni yule ambaye baada ya kutimuliwa Dar es salaam, aliibukia Morogoro ambako aliendeleza staili yake ya kuomba akiwa amelala chali huku mkono akiwa ameunyoosha juu kwa muda mredfu bila ya kutikisika hata kama jua ni kali kupita kiasi.
Kijijini, Matonya anaishi kwenye nyumba ya tembe ambayo ni mali ya mtoto wake wa kike aitwaye Elizabeth Matonya.
Nyumba hiyo ya asili ya watu wa Dodoma ipo kwenye Kijiji cha Bahi Sokoni katika Kitongoji cha Nghungugu, umbali wa kilomita 3 kutoka yalipo makao makuu ya wilaya ya Bahi.
Kwa hisani ya Juma Mtanda Morogoro.
No comments :
Post a Comment