Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi wakati wa Uhaiwake akiwa kwenye majukwaa yakimataifa.Waziri Mkuu huyo uatawalawake ulikuwa na utata mwingi hasa kwa vyombo vya habari.
Meles Zenawi alipokuwa Hospitalini baada ya afyayake ilipozorota. |
Mjue Zenawi na kifo chake.
TAARIFA ya baraza la mawaziri imesema
kuwa Zenawi alikuwa akipata matibabu ng'ambo na afya yake ilikuwa ikiimarika
lakini akazidiwa siku ya Jumapili alipolazimika kurejeshwa hospitali,
''Ingawaje madaktari wake walifanya kila wawezalo, alifariki jana mwendo wa
23:40,'' taarifa hiyo imesema.
Bwana Zenawi alikuwa kiongozi wa
Ethiopia wakati taifa hilo lilipoingia vitani na nchi jirani ya Eritrea mwaka
1998.Meles Zenawi aliingia mamlakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi lakini
akapokea sifa kutoka kwa mataifa ya magharibi.
Waziri mkuu wa Kenya raila Odinga
ameiambia BBC kuwa ana hofu kuhusu hali nchini Ethiopia kufuatia kifo cha Meles
Zenawi.Alisema kuwa hali nchini humo sio nzuri huku vita vya kikabila
vikiendelea kuwa tishio.
Bwana Odinga alimtaja Zenawi kama
kiongozi mashuhuri na mwenye elimu bora, aliyejitolea kuunganisha bara la
afrika.Naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn anatarajiwa kuchukua mahala pake
No comments :
Post a Comment