NEW YORK, Marekani
MCHEZA
Tenisi mahiri Rafael Nadal, amelazimika kujitoa kwenye Mashindano ya
Wazi ya Marekani (US Open) yanayotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu,
kutokana na jeraha la goti linaloendelea kumtesa.
Nadal, 26, nyota huyo wa kimataifa wa Hispania, pia alishindwa kuwa
sehemu ya washiriki wa mashindano ya Olimpiki jijini London iliyofikia
tamati hivi karibuni kwa tatizo hilo na hajacheza michuano yoyote tangu
alioposhiriki Wimbledon.
Nyota
huyo anayeshika nafasi ya tatu ya viwango vya ubora wa mchezo huo
duniani, ambaye alishinda Grand Slams jijini New York mwaka 2010, pia
alishindwa kucheza Masters Series huko Toronto na Cincinnati, lakini
sasa ana matumaini ya kucheza Flushing Meadows.
Nadal alisema: “Ninasikitika sana
kutangaza rasmi kwamba, bado siko tayari kucheza tenisi na hivyo
nalazimika kujitoa katika Mashindano ya Wazi ya Marekani yatakayofanyika
kuanzia Agosti 27, jijini New York mwaka huu.
“Nasikitika
kuwa nitaendelea kukosa kucheza mashindano makubwa yenye uungwaji mkono
mkubwa, lakini naendelea na maandalizi ya kuhakikisha narudi vema
mchezoni nikiwa kwenye hali stahili.
“Napenda
kusema shukrani kwa mashabiki wangu wote, hasa wa mashindano ya New
Yorke. Nitawakosa kwa mwaka huu wa mashindano hayo ya wazi!”
Mkurugenzi
wa Mashindano ya US Open, David Brewer aliongeza: “Rafael amewasiliana
nasi kututaaruifu kuwa hayuko fiti kushindana katika mashindano ya mwaka
huu na kwamba ameamua kujitoa katika michuano hiyo.
“Tuna
matumaini makubwa ya kumuona akirejea tena viwanjani na kumuona
akiangalia mbele zaidi kuelekea mashindano ya mwakani ya US Open hapa New York."
Mashindano ya US Open yanatarajia kuanza kutimua vumbi hapo Agosti 27, huku wakali kama
Roger Federer na Novak Djokovic wakiwa miongoni mwa nyota wa kiume
watakachuana, wakati David Ferrer akitarajiwa kupanda hadi nafasi za
juu.
No comments :
Post a Comment