Na Mwandishi Wetu
MABONDIA wakongwe nchini, Rashid Matumla 'Snake Man' na Maneno Oswald 'Mtambo wa Gongo', watapigana pambano la kustaafishana siku ya Idd Mosi kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar es Salaam.
MABONDIA wakongwe nchini, Rashid Matumla 'Snake Man' na Maneno Oswald 'Mtambo wa Gongo', watapigana pambano la kustaafishana siku ya Idd Mosi kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar es Salaam.
Pambano hilo limeitwa la kustaafishana kwa sababu, bondia mmoja
atakayepigwa, atatakiwa kustaafu ngumi kutokana na makubaliano ya
pambano hilo.
Mratibu wa burudani wa Dar Live, Luqman Maloto, aliwaambia
waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa, Matumla na Maneno
watapigana pambano la raundi 10, kisha litafuatiwa na mambano mengine
mawili na atakayepigwa atastaafu ngumi.
"Mabondia wenyewe ndiyo walitaka kuwe na pambano la aina hiyo, kwa
hiyo mashabiki wao waje kwa wingi siku ya Sikukuu ya Idd Mosi Dar Live
ili wapate picha ni nani kati ya mabondia hao anaweza kustaafu.
"Siku hiyo itakuwa ni uzinduzi mpya wa Ukumbi wa Dar Live, kwa hiyo
kutakuwa na shoo kali ya muziki wa kizazi kipya kutoka kwa wanamuziki
wakali, Mwasiti Almasi, Maunda Zorro, Estelina Sanga 'Linah', Mzee Yusuf
akiwa na kundi zima la Jahazi Modern Taarab bila kumsahau Juma Nature
na TMK Wanaume Halisi pia atakuwepo," alisema Maloto.
Kwa upande wa mabondia hao, kila mmoja ametamba kumchakaza na
kumstaafisha mwenzake, wakati wanamuziki hao, nao wakiahidi kutoa
burudani ya nguvu kwa ajili ya siku hiyo ya furaha baada ya mfungo wa
mwezi mtukufu wa Ramadhani.
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana
mbalimbali
No comments :
Post a Comment