Mkurugenzi
Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei akikata utepe wakati wa ufunguzi wa
tawi jipya la benki hiyo lililopo Tegeta nje kidogo ya jiji la Dar es
Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa tawi hiyo, Daudi
Nyandwi. Wa tatu kushoto ni Naibu Mkurugenzi Huduma Shirikishi wa CRDB,
Esther Kitoka na Mkurugenzi Mkuu wa VGK, Velence Msaki.
Karibu Bosi.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Nenki ya CRDB, Tully Mwambapa (kulia), akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Karibu katika tawi letu.
Mkurugenzi Mkuu wa VGK, Velence Msaki (kushoto), akiwa na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya wageni walioshiriki uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la Tegeta jijini Dar es Salam.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Nenki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kushoto), akiwa na Meneja wa Huduma kwa Wateja, Godwin Semunyo wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Nenki ya CRDB, Tully Mwambapa (wa Pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NMB mara baada ya uzinduzi wa tawi la CRDB ambalo lipo katika jengo la KIBO COMMERCIAL COMPLEX ambapo benki ya NMB imefungu tawi katika jengo hilo.
DAR ES SALAAM, Tanzania
WATANZANIA wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuweka katika miradi mikubwa ili kujikomboa kimaisha.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Vijijini CRDB,Dkt.Charles Kimei wakati akifungua la biashara la Kibo Commercial Complex lililopo Tegeta,Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambalo limejengwa kwa udhamini wa Benki hiyo ya CRDB.
Alisema Watanzania wengi wamekuwa wakihofia kuwekeza katika miradi mikubwa kutokana na kwamba wanashindwa kufanya kazi kwa bidii jambo ambalo limekuwa likiwapa fursa wageni kutoka nje ya nchi.
"Watanzania wengi wamekuwa na hofu katika kuwekeza katika miradi mkubwa na hofu hii inatokana kwamba washindwa kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii,"alisema Dkt. Kimei.
Alisema kuwa uoga huo unatokana na kutokuwa na nidhamu katika kutunza fedha benki jambo ambali linawafanya kushindwa kupata mikopo.
Mkurugenzi huyo Mtendaji alisema kuwa endapo watanzania wataondokana na hali hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kujikwamua kimaisha.
Awali akisoma hotuba yake kwa mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo ya VGK Ltd.Bw. Valence Msaky,pamoja na changamoto mbalimbali walizokutana nazo lakini wanashukuru kuona wamefanikisha ujenzi huo.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kupatikana fedha za ujenzi,imene wa uhakika,mfuko wa bei za bidhaa na uagizaji wa vifaa kutoka nje ya kutofika kwa watakati.
No comments :
Post a Comment