Mwakilishi
wa Jumuia ya Afrika Mashariki katika Umoja wa Nchi huru za Afrika,
Filbart Magere (kulia) akimkabidhi kikombe Ibrahim Obuta, baada ya timu
kuibuka mshindi wa wachezaji mmoja mmoja (singles) katika mashindano ya Vishale(Darts) ya Afrika Mashariki ya yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
Wachezazi
wa Darts upande wa wanawake wakishangilia ushindi wao baada ya kutwaa
ubingwa wakati wa mashindano ya mchezo huo ya Afrika Mashariki
yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
*********************
Na Mwandishi Wetu
TIMU
ya mchezo wa Vishale (Darts) ya wanaume kutoka nchini Kenya imetwaa
ubingwa wakati wa fainali ya mashindano ya Kimataifa ya Afrika mashariki
yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Monarch jijini
Mwanza na kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu shilingi laki mbili.
Wakenya
walitwaa Ubingwa huo kwa kuwagalagaza watanzania katika kiwango cha
juu hivyo kuwadhihilishia kuwa Tanzania wanahitaji mazoezi ya kutosha
ili kufikia kiwango chao cha maechi za kimataifa ili kupata uzoefu
zaidi.
Akizungumza
na wachezaji wakati wa kukabidhi zawadi mgeni rasmi ambaye ni
mwakilishi wa jumuia za Afrika Mashariki katika Umoja wa nchi huru za
Afrika, Flilbart Magere, aliwapongeza wachezaji wa timu hiyo kutoka
Kenya kwa kutwaa Ubingwa na pia wachezaji wote walioshiriki mashindano
hayo.
Magere
alisema kuwa mchezo huo wa vishale sasa unazidi kupata umaarufu na hasa
Afrika mashariki hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anafanya
kila jitihada za kuuinua mchezo huo na kuutangaza ili upate wachezaji na
wapenzi wengi.
Aidha aliipongeza Tanzania kwa kuandaa mashindano hayo ya Vishale ngazi ya Kimataifa.
Magere
pia aliipongeza Kampuni ya Bia Tanzani(TBL) kupitia Bia yake ya Safari
Lager kwa kufadhili mashindano hayo na pia aliyaomba makampuni mengeni
kuiga mfano wa kampuni hiyo.
Washindi
wa pili wanaume katika mashindano hayo ya Afrika Mashariki walikuwa
Lugalo ya Tanzania ambao walipata pesa taslimu shilingi laki mbili
wakati upande wa Wanawake nafasi ya kwanza ilichukuliwa pia na timu ya
Nyerere kutoka Tanzania, ambayo ilizawadiwa kikombe na pesa taslimu
shilingi laki mbili na nafasi ya pili ni Utawala ya Kenya ambayo
ilizawadiwa shilingi laki moja.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Ibrahim
Obuta kutoka Kenya ambaye alizawadiwa kikombe na pesa taslimu shilingi
laki mbili na wa pili ni Wambura Msira kutoka Tanzania ambaye
alizawadiwa pesa taslimu shilingi laki moja,
Kwa
upande wa singles wanawake nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Rosemary
Wanyori, kutoka Kenya ambaye alizawadiwa kikombe na pesa taslimu
shilingi laki moja na wa pili ni Amoding Dinah, kutoka Uganda ambaye
alizawadiwa pesa taslimu shilingi laki moja.
No comments :
Post a Comment