Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, July 2, 2012

Airtel yaja na "Kula Dabo" ndani ya saba saba

 Meneja Uhusinao wa Airtel, Jackson Mbando, akizungumza katika uzinduzi wa promotion kabambe kwa wateja wao ijulikanayo kama “kula Dabo”  kupitia huduma ya Airtel Money. Uzinduzi wa promotion hiyo ameufanya leo katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam(DITF) maarufu Saba Saba yanayopendelea katika barabara ya Kilwa jijini.
 Meneja Uhusinao wa Airtel, Jackson Mbando,(aliye chuchuma mbele) akipiga picha ya pamoja na baadhi ya vijana wanaotoa huduma mbalimbali katika banda la Airtel, baada ya uzinduzi wa promotion kabambe kwa wateja wao ijulikanayo kama “kula Dabo”  kupitia huduma ya Airtel Money. Uzinduzi wa promotion hiyo ameufanya leo katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam(DITF) maarufu Saba Saba yanayopendelea katika barabara ya Kilwa jijini. .
 Meneja Uhusinao wa Airtel, Jackson Mbando, akizungumza katika uzinduzi wa promotion kabambe kwa wateja wao ijulikanayo kama “kula Dabo” pia alimpigia simu mteja mmoja mara baada ya kuibuka mshindi wa zawadi za papo kwa papo ndani ya saba saba. Uzinduzi wa promotion hiyo ameufanya leo katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam(DITF) maarufu Saba Saba yanayopendelea katika barabara ya Kilwa jijini. Kulia ni Ofisa wa Airtel Money, Bahati Straton
Afisa wa Airtel 3G, Teher Abdulrahman, akichagua kikaratasi cha mshindi katika  Bahati nasibu ya Papo kwa Papo katika viwanja vya sabasaba ndani ya Kijiji cha Airtel. Kushoto ni Meneja Uhusinao wa Airtel, Jackson Mbando na Katikati ni Ofisa wa Airtel Money, Bahati Straton, Airtel pia ilizindua promotion ya “Kula Dabo” kwa wateja wao watakao nunua bidhaa kwa Airtel Money.

KAMPUNI ya simu za mkono ya Airtel Tanzania jana imezindua promosheni kwa wateja inayojulikana kama “Kula Dabo” katika maonyesho ya 36 ya biashara kwenye viwanja vya Sabasaba Temeke.

Akizindua promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa kampuni ya Airtel, Jackson Mmbando alisema kuwa katika kuhakikisha huduma ya pesa mkononi inamfikia kila Mtanzania na kupunguza changamoto mbalimbali za kifedha.

Alisema kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imeamua kuwazawadia wateja wake wote wanaonunua salio kupitia simu za mknoni kupata mara mbili ya salio lolote atakaloongeza kupitia Airtel Money na ataweza kupiga simu na kutuma sms kwenda mtandao wowote
Promosheni hii itaendelea katika msimu huu wa sabaSaba ambapo itadumu kwa muda wa wiki mbili kuanzia sasa, Mmbando alisema “ Airtel kwa kuonyesha tunawajali wakala wetu wote, mwezi huu kila wakala atapata mara mbili ya kamisheni yake, lengo letu ni kuhakikisha kila mdau wetu anafaidika na huduma yetu hii ya Airtel money”  

“Wakala wetu sasa mnakila sababu ya kuhakikisha mwezi huu unafanya mhamala mingi ili tu muweze kupata kamisheni nyingi kwa kula dabo yako” aliendelea kusema Mmbando
Vilevile mbali na kuwepo kwa promosheni ya kula dabo wateja wa Airtel watakaonunua bidhaa mbali mbali katika viwanja na banda lete la sabasaba kupitia huduma yetu ya Airtel money wataweza kujishindia zawadi mbali mbali ikiwemo pesa taslim kuanzia shilingi 2,000, simu za mkononi aina ya Samsung 1085 pamoja na modem ya 3.75G kupitia droo ya kuchanganya kuponi itakayofanyika katika viwanja hivyo kila siku saa nane kamili.

Airtel tunawakaribisha wateja wetu kutembea kijiji cha Airtel katika Maonyesho ya 36 ya biashara ambayo yataendelea kwa muda wa siku kumi ili kujipatia huduma zetu mbali mbali ikiwemo ya Airtel Money, kuwezesha simu yako kutumia intaneti yenye spidi, kujipatia modem za 3.75G kwa gharama nafuu zaidi pamoja na kujua huduma nyingine nyingi kutoka Airtel.

Airtel hivi karibuni ilizindua na kuboresha huduma ya Airtel Money pesa mkononi na mpaka sasa watanzania wengi wamenufaika kwani imeweza kutoa ajira kwa watanzania wengi  kwa kupitia uwakala hivyo wananchi wengi wameweza kujipatia mapato kwa kupitia huduma hii, kwa wateja wetu wote Airtel money ina mawakala zaidi ya 10,000  waliosambaa nchi nzima na kupitia huduma ya Airtel Money unaweza kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao wowote nchini na utaweza kutuma kuanzia shilingi 1,000 hadi kiwango cha shilingi 1,000,000 kwa Airtel money.

Maonyesho ya kimataifa ya Dar es salaam Maarufu kama sabasaba, Ni maonesho ya kibiashara yanayoongoza Tanzania maonyesho hayo yanayofanyika kwa siku kumi huvutia wageni zaidi ya milioni nne na kujenga mahusiano na maingiliano baina ya watoa huduma na wateja wao na kutoa fursa kwa wateja kuangalia na kulinganisha ubora wa bidhaa.
x

No comments :

Post a Comment