Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou akiwasili katika
banda la Mfuko wa Fursa Sawa kwa wote (EOTF) wakati wa maonyesho ya 36
ya Kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea.Kushoto ni Afisa Mawasaliano
wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu.
Mwenyekiti
wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa (kulia)
akimkaribisha Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic
Kacou (kushoto) katika banda la mfuko huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa (EOTF ) Bw. Stephen Emmanuel (kulia) akisalmiana na Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou. Katikati ni
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou akitia saini kitabu cha
wageni katika banda la mfuko wa fursa sawa kwa wote (EOTF).
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou akikagua moja ya
bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali kutoka bara na visiwani ambao
wamepewa mafunzo na mfuko huo kabla ya kushiriki maonyesho hayo. Wa pili
kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa (EOTF ) Bw. Stephen Emmanuel ,
Mwenyekiti wa Mfuko huo Mama Anna Mkapa pamoja na Afisa Mawasiliano wa
Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu.
Dkt.
Alberic Kacou akitazama Juisi asilia ambao haijachanganywa na kemikali
yoyote zinazotengenezwa na kikundi cha Wajasiriamali wa KYM'S
ENTERPRISES cha Kibaha wanaopatikana katika banda la mfuko wa Fursa Sawa
kwa wote (EOSF).
Katika
ziara hiyo Dkt. Alberic Kacou alikutana na Waziri wa Viwanda na
Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (Kushoto) alipotembelea banda la mfuko wa
Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou akitazama
chakula cha aina ya Senene kilichofungashwa na majani maalum ya Mgomba,
Chakula hicho ni maarufu kwa wenyeji wa mkoa wa Kagera.
Afisa
Mipango wa (EOTF) Bi. Rehema Batakanwa(kulia) akitoa maelezo bidhaa za
Vitenge vinavyotengenezwa na Maare Enterprises kwa Dkt. Alberic Kacou
(katikati) wakati wa ziara yake katika Banda la mfuko wa fursa sawa kwa
wote (EOTF). Kushoto ni Mkurugenzi wa Maare Enterprises Bi. Florence
Maare.
Dkt. Alberic Kacou akionekana kuvutiwa moja ya bidhaa katika banda hilo.
Meneja
Mauzo na Masoko wa Moring Natural Products Christina Ngoti (kulia)
akitolea maelezo ya dawa ya asili isiyonakemikali aina ya Mlonge
inayotibu Mangonjwa 300 kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania
Dkt. Alberic Kacou (katikati). Kulia ni Afisa Mipango wa (EOTF) Bi.
Rehema Batakanwa.
Dkt.
Ableric Kacou (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti Mtendaji wa
IPP Dkt. Reginald Mengi pamoja na Mwenyekiti wa mfuko wa Fursa sawa kwa
wote (EOTF) Mama Anna Mkapa (katikati) wakati alipotembelea banda hilo
katika maonyesho ya 36 ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya
Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou (katikati)
akiagana na Mwenyekiti wa mfuko wa Fursa sawa kwa wote Mama Anna Mkapa
baada ya kumaliza kutemebelea mabanda ya wajasiriamali waliowezeshwa na
mfuko huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa (EOTF ) Bw. Stephen Emmanuel.
No comments :
Post a Comment