Aliyewahi kuwa bingwa wa dunia wa mita 800, binti Semenya kutoka Afika Kusini anatarajiwa kubeba bendera na kukiongoza kikosi cha Afrika Kusini katika sherehe za uzinduzi wa michuano ya Olympic, mjini London.
Chama
cha michezo Africa Kusini pamoja na kamati ya Olympic (Sascoc) walitoa
tangazo hilo siku ya jumatano katika sherehe za kuiaga timu hiyo kabla
ya kuelekea London.
Ikiwa
amezaliwa katika kijiji kidogo cha GaMasehlong huko Limpopo, Semenya
alishinda taji la dunia katika mashindano ya kimataifa ya riadha kwa
mita 800, mjini Berlin, Germany, mwaka 2009. Wakati huo akiwa na umri wa
miaka 18 tu.
No comments :
Post a Comment