Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, July 4, 2012

Warembo 15 wamejitokeza kuwania taji la Mrembo wa Sinza




JUMLA ya warembo 15 wamejitokeza  kuwania taji la Mrembo wa Sinza “Redds Miss Sinza 2012” yaliyopangwa kufanyika julai 13 kwenye ukumbi wa Mawela social (Ten Star  Lounge) uliopo karibu na hotel ya Vatican City.

 
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary wa kampuni ya Calapy Entertainment aliwataja warembo hao kuwa ni Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Eva Mushi, Vailet John, Esther Mussa, Christina Samwel, Nahma Said, Shadya Ali, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.

Majuto alisema kuwa warembo hao wapo kambini chini ya mwalimu wao, Mwajabu Juma ambaye kwa sasa anashikilia taji la Miss Tanzania Top Model. Alisema kuwa mazoezi ya warembo hao yanafanyika kwenye ukumbi wa mashindano hayo, Mawela social kuanzia saa 8.30 mchana.

“Warembo wamepania kufanya kitu cha kihistoria siku ya mashindano nah ii inatokana na ukweli kuwa wamejiandaa vilivyo na kwa sasa wanamalizia tu baadhi ya vitu vidogo vidogo vya mashindano hayo, alisema Majuto.

Alisema kuwa lengo kubwa la mashindano ya mwaka huu ni kutwaa taji la Redds Miss Tanzania mbali ya taji la Kanda ya Kinondoni katika shindano hilo lililodhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Kidoti Fashion, Clouds Entertainment, sufianimafoto.blogspot.com, Lady Pepeta na flexi P, Fredito Entertainment, Screen Masters, Brake  Point na Jackz Cosmetics Kinondoni.

“Tuna warembo moto wa kuotea mbali ambao kwa sasa wameonyesha kupania kufanya kile ambacho kimesubiliwa na wadau wa warembo wa mitaa ya Sinza na vitongoji vyake, hii inatokana na ukweli kuwa mashindano haya ni ya mwisho kwa upande wa vitongoji jijini,” alisema.

No comments :

Post a Comment