Treni ikiteketea kwa moto wakati juhudu za uokozi zikiendelea
WATU
zaidi ya 30 wameuawa Kusini mwa India katika mji wa Chennai kwa
kuteketea kwa moto baada ya gari moshi walilokuwa wanasafiria kuwaka
moto Julai 30, 2012.
Mkasa
huo umetokea Jumatatu asubuhi wakati gari moshi hilo lilipokuwa
linatokea mjini New Delhi na kusababisha abiria wengine zaidi ya 20
kujeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.
Maafisa
wa uokoaji kwa sasa wanaendelea na shughuli za kuwatafuta watu zaidi
ambao huenda wamekwama ndani ya gari moshi hilo huku idadi ya wafu
ikitarajiwa kuongezeka.
Walioshuhudia
mkasa huo wanasema, waliona gari moshi hilo likiwaka moto likiwa
safarini, mkasa ambao umeleta kumbukumbuku ya ajali nyingine ya gari
moshi iliyotokea mwezi Mei mwaka huu baada ya magari Moshi kugongana na
kusababisha zaidi ya watu 20 kuuawa.
Taasisi
inayoshughulika na maswala ya ajali za terni nchini humo inasema kuwa
tangu mwaka 2009, watu 25,705 wameuawa kutokana na ajali za gari
moshi.
Ajali
mbaya zaidi ya gari moshi iliyowahi kuikumba nchi hiyo ilikuwa mwaka
1981 ambapo watu 800 waliuawa baada ya gari moshi la abiria kuzama
katika mto katika jimbo la Bihar.
Serikali ya India inasema iko katika harakati za kuimarisha sekta ya safari za reli kwa kuimarisha usalama wa magari moshi.
No comments :
Post a Comment