Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, August 8, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL, AFUNGA MAONYESHO YA SHEREHE ZA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE MJINI DODOMA



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi kikombe Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatuma Salum Ally, baada ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kuwa mshindi wa jumla katika maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo, wakati alipokuwa akifunga maonyesho hayo  katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mmoja kati ya wajasiliamali wa vikundi vya wakulima, wakati alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo,  katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili wakati walipowasili kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma leo, kwa ajili ya kufunga rasmi maonyesho hayo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipomwakilisha Rais Jakaya Kikwete, kufunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo, katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha Tuzo aliyokabidhiwa kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Rais katika kusimamia na kuendeleza Kilimo Kwanza, wakati Makamu alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma leo. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza.

No comments :

Post a Comment