Pichani kati ni Mwanamuziki mahiri Josee Mara akifafanua kuhusiana na
mikakati yao waliyonayo kwa sasa mara baada ya mwanamuziki mwenzao
mmoja,Kalala Jr kutimka na kuwaacha wakiwa wawili badala ya watatu.Josee
Mara amesema wao wako fiti na hakuna kilichoharibika,kwani kuna
wanamuziki wengine kadhaa ambao ni wazuri na watafanya nao kazi kama
ilivyokuwa kwa Kalala Jr."Na sasa hivi nakuhakikishia Da'Suzzy tutapiga
kazi ile mbaya,kwa sababu hao vijana tunaowaongeza ni wanamuziki wazuri
na tunawahamu toka kitambo,kwa hivyo naamini mambo yatakuwa sawa na
washabiki wetu wasivunjike moyo,waendelee kutuunga mkono tu,sisi ni
wapambanaji kwa hiyo ni lazima tupambane"amesema Josee Mara.Aidha Khalid
Chokoraa ameongeza kuwa katika kuonesha bado wako fiti wamekwisharekodi
singo yao moja iitwayo ONA NAONEWA,ambayo wataitambulisha hivi
karibuni kwa mashabiki wa muziki wa dansi
Mmoja wa watangazaji wa Clouds FM,kupitia kipindi cha Wikend Bonanza,Da'
Suzzy akizungumza na wanamuziki mahiri wa dansi hapa nchini waliokuwa
wakijiita Mapacha 3,ambapo kwa sasa mmoja wao Kalala Jr ameamua kuachia
ngazi na kuwaacaha wenzake Khalid Chokoraa na Josee Mara kama uwaonavyo
pichani wakiwa na Meneja wao Hamis Dacota pichani kulia.Da'Suzzy alikuwa
akitaka kujua kwanini msanii mwenzao Kalala Jr ameamua kutimka kwenye
bendi yao na kwamba wana mikakati gani ya kuliziba pengo la mwanamuziki
huyo aliyetimka.Kwa mujibu wa Meneja wa bendi hiyo ya Mapacha 3,Hamis
Dacota amebainisha kuwa Kalala Jr aliamua kuondoka mwenyewe bila kuwepo
na ugomvi wowote baina yao,"hivyo kama mwanamuziki mwenzetu,kijana
mwenzetu tunamtakia kila kheri huko aendako,lakini kama akitaka kurudi
pia milango iko wazi anakaribishwa sana,kwa sababu yeye ni mmoja wa
waasisi wa bendi ya mapacha 3",alisema Dacota.
No comments :
Post a Comment