Mkurugenzi
Mtendaji wa Muunganiko wa Makampuni ya BancABC, Douglas Munatsi (kulia)
akimkabidhi kombe Makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani kwa ajili ya mashindano ya
BancABC SUP8R wakati wa uzinduzi rasmi uliofanyika Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Bingwa
wa michuano ya BancABC Super 8 inayoanza keshokutwa (Agosti 5 mwaka
huu) katika miji ya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza na Arusha atapata
sh. milioni 40 wakati makamu bingwa sh. milioni 20. Pia timu mbili
zitakazoishia hatua ya nusu fainali kila moja itapata sh. milioni 15
wakati zilizobaki kila moja itapata sh. milioni 5.
Timu
zimepangwa katika makundi mawili ya A na B. Kundi A lina timu za Simba
(mabingwa wa Tanzania Bara), Jamhuri, Zimamoto na Mtende zote za
Zanzibar. Kundi ni Super Falcon (mabingwa wa Zanzibar), Azam, Mtibwa
Sugar na Polisi Morogoro zote za Tanzania Bara.
Mechi
za ufunguzi keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) ni Simba vs Jamhuri (Dar es
Salaam), Zimamoto vs Mtende (Mwanza), Mtibwa Sugar vs Polisi Morogoro
(Arusha) na Super Falcon vs Azam (Zanzibar). Awali mashindano yalikuwa
yaanze Agosti 4 mwaka huu lakini yamesogezwa mbele kwa siku moja.
Hatua ya makundi itamalizika Agosti 12 mwaka huu. Mechi za nusu fainali na fainali zote zitachezwa Dar es Salaam.
Mdhamini
bancABC atagharamia usafiri wa ndege kwa timu zote kutoka kituo kimoja
hadi kingine, malazi na jezi. Yanga imejitokea kwenye mashindano hayo na
nafasi yake imechukuliwa na Mtibwa Sugar ambayo ilishika nafasi ya nne
kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.
No comments :
Post a Comment