Mkuu
wa Idara ya Oganizesheni na Siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma (kulia)
akimkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa,
Innocent Melleck katika ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Vijana jijini
Dar es Salaam.
Na Andrew Chale
KADA
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Umoja wa Vijana wa (UVCCM),
Innocent Melleck, amejitosa kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Makamu
Mwenyekiti Taifa wa UVCCM Tanzania Bara.
Mellack alichukua fomu hiyo jana kwenye ofisi za makao makuu ya UVCCM jijini Dar es Salaam na kusema kuwa yeye ni miongoni mwa watoto wa mkulima, hivyo kuchukua fomu na kuwania nafasi hiyo anawakilisha vijana hao.
“Nimechukua
fomu nikiwa miongoni mwa watoto wa mkulima na kuwawakilisha vijana wote
wa Tanzania, nitahakikisha narudisha hadhi UVCCM, na pia kuujenga umoja
huu kuwa wa hadhi,” alisema.
Aidha, alisema kugombea kwake hajashawishiwa na mtu na wala hana makundi ndani ya umoja huo, kwani anachohitaji ni kuleta mabadiliko ya kweli na kuondoa ubinafsi uliojijenga kwa muda mrefu.
Melleck
alikabidhiwa fomu hiyo na Mkuu wa Idara ya Oganizesheni na Siasa UVCCM,
Taifa, Sophia Duma, ambapo alitakiwa kuirejesha baada ya kuijaza na
mwisho wa kurudishwa ni Agosti 6.
No comments :
Post a Comment