Naibu katibu mkuu wa
UVCCM Zanzibar, Jamal Kasim Ally akimkabithi fomu za kugombea nafasi ya
uongozi wa UVCCM-NEC Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Bw Jerry Silaa
jana katika
ofisi za CCM mkoa mjini magharibi Zanzibar, (ktk) mwenye suti nyeusi ni
Bw Abdallah Mwinyi-katibu wa vijana mkoa kusini unguja akishuhudia
tukio hilo. UVCCM -NEC imetangaza nafasi zinazogomewa kua ni Mwenyekiti,
Mkamu mwenyekiti, Katibu, wajumbe wa baraza kuu na wajumbe wa
halmashauri. Hata hivo mstahiki meya wa manispaa ya ilala alipohojiwa
hakuweka wazi nafasi gani anayotaka kugombea kwani alikua bado
anakusanya maoni na ushauri kutoka watanzania mbalimbali na kujipima
mwenyewe ni nafasi ipi itakayo mfaa zaidi ili kuweza kuwatumukia
wananchi vema.Tetesi kutoka kwa wadau wake wa karibu zinasema mstahiki
meya anataka kugombea nafasi ya Mwenyekiti UVCCM-NEC.
UWT KIBAHA MJI YAFANYA KWELI YAADHIMISHA MIAKA 49 YA CCM KWA KUPANDA MITI
-
Jumuiya ya umoja wa wanawake Wilaya ya Kibaha mjini (UWT) katika kusherekea
maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi (CCM) kimeamua ...
9 hours ago
No comments :
Post a Comment