Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, August 9, 2012

DART yaingilia mahakama kuhusu Wahanga wa bomoabomoa ya Gerezani


Thursday, August 9, 2012



Na Mwandishi Wetu

WANANCHI na wahanga wa bomoabomoa kwa wakzi wa nyumba za kota za eneo la Gerezani, Kariakoo, Dar es Salaam, wametahadharishwa kuacha kuchukua hatua yoyote kutokana na suala lao kuwa mahakamani.
Wahanga hao wanasubiri kujua kama watafidiwa kitu chochote kutokana na bomoabomoa iliyowakumba hivi karibuni, na kupata fidia ya uharibifu na uvunjifu wa haki za wakazi hao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wakili Sengondo Mvungi, anayelisimamia suala hilo, alisema wakazi hao wanatakiwa kuwa watulivu kwa sasa wakati suala lao likishughulikiwa kisheria, huku akiwaahidi kulisimamia ipasavyo.
Mvungi, ambaye anatoka katika ofisi ya mawakili ya South Law Chambers, alisema suala lao litashughulikiwa bila kuwa na tatizo lolote likisimamiwa na yeye, na kuwasihi wanachi na wakazi wa eneo hilo kuwa na subira.
Alisema: "Suala la haki ya umiliki tajwa na fidia itokanayo na utwaaji wa eneo hilo na Serikali na fiudia ya uharibifu na uvunjifu wa haki za binadamu za wakazi wa Gerezani ziko mahakamani kwa mujibu wa kesi namba 44 ya mwaka 2012."
Mvungi, alisema taarifa zilizotajwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Haraka (DART) kwa wahanga wakapokee fidia zao linakiuka amri ya Mahakama Kuu, iliyotajwa Juni 28, 2012, na kuwashauri kutotii agizo hilo.
Aidha, wakili huyo anayewasimamia wananchi wa Gerezani, amewataka kuhudhuria katika kikao cha pamoja na wakili wao (Mvungi), kitakachofanyika Agosti 11 mwaka huu (Jumamosi) katika ukumbi watakaoarifiwa na kamati.

No comments :

Post a Comment