Jaji Warioba: Wananchi Wasilazimishwe kutoa Maoni na Vyama vya Siasa, Taasisi za Kidini na Wanaharakati
Na Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam
Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba avitaka vyama vya
siasa, asasi za kidini na wanaharakati kuacha kuwaelekeza wananchi aina ya
maoni wanayopaswa kutoa kuhusu Katiba Mpya.
Jaji
Warioba ameyasema hayo leo (Alhamisi, Agosti 9, 2012) katika mkutano wake na
waandishi wa habari kuzungumzia tathmini ya mikutano ya awamu ya kwanza ya
ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya katika mikoa minane ya Pwani,
Dodoma, Manyara, Kagera, Shinyanga, Tanga, Kusini Unguja na Kusini Pemba.
“Sio
wanasiasa tu, watu wote wakiwemo viongozi wa kidini, wanaharakati na taasisi
zisizo za kiserikali ziache kuwalazimisha wananchi watoe maoni wanayotaka wao.
Wananchi wawe huru kutoa maoni yao,” alisema na kuongeza kuwa vyama vya siasa,
asasi zisizo za kiserikali ziatapata muda wa kuwasilisha maoni yao Tume.
“Mwananchi
akitoa maoni yake binafsi, anakuwa ‘very articulate’ (anajieleza kwa ufasaha),
lakini akielekezwa cha kusema, na ukamuomba ufafanuzi, anashindwa hata kueleza,”
alisema Jaji Warioba katika mkutano huo uliohudhuriwa na pia na Katibu wa Tume
hiyo, Bw. Assaa Rashid na Naibu Katibu Bw. Casmir Kyuki.
Kuhusu
idadi ya mikutano iliyofanyika katika awamu ya kwanza, Mwenyekiti huyo amesema
Tume yake imefanya mikutano 386 katika mikoa minane ya awamu ya kwanza kwa muda
wa mwezi mmoja
No comments :
Post a Comment