Mwandishi Wetu
MABINGWA wa kombe la
Kagame, Yanga kwa kushirikiana na kampuni ya Push Media Mobile wamekabidhi
zawadi za bajaj na pikipiki kwa mashabiki wa timu hiyo walioshinda katika
bahati nasibu inayojulikana kwa Young Africans loyalty SMS campaigns for 2012.
Washindi hao ambao walitangazwa rasmi katika mechi ya ya
fainali ambayo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC na
kutwaa kombe hilo kwa mara ya pili ni Roby Revecatus kutoka Mwanza na Amir
Jafari (Tabora) ambao walikabidhiwa pikipiki kila mmoja na Finyasi Vincent
aliyeshinda bajaj.
Mabashabiki hao walikabidhiwa zawadi zao makao makuu ya klabu
ya Yanga, Jangwani na Afisa Habari wa klabu hiyo Louis Sendeu na meneja wa shindano
hilo, Talib Rashid kutoka kampuni ya Push Mobile.
Rashid alisema kuwa wamefarijika kukabidhi zaidi hizo ambazo
zimekwenda sambamba na shamrashamra na ushindi wa timu hiyo.
Alisema kuwa kampuni yao iliendesha shindano hilo kwa lengo
la kuwapa ufahamu zaidi mashabiki wa timu hiyo kuhusiana na historia ya Yanga
na mambo mengine muhimu ya klabu hiyo.
“Baada ya Bajaj na pilipiki, shindano linalokuja litakuwa la
kuwania gari, hivyo nawataka kukaa mkao wa kula ili kushiriki katika shindano
hilo,” alisema Talib.
Naye mshindi wa Bajaj, Finyiasi Vicent aliipongeza Push
Mobile na Yanga kuendesha bahati nasibu hiyo ambayo imewafanya wao kusheherekea
pamoja na ubingwa wa timu hiyo.
“Ni faraja kwetu kwa kukadhiwa zawadi zetu sambamba na
ushindi wa kombe la Kagame, mimi na wenzangu tunajiona kuwa wenye bahati kubwa
kwa kupata fursa hii,” alisema Vincent.
You might also like:
No comments :
Post a Comment