Washindi wa Castle Lager Super fan Yahaya
 Hamza toka mkoani Mwanza na Filbert Nestory toka Dar Es Salaam wakiwa 
na Meneja wa Bia ya Castle lager Kabula Nshimo kwenye kikao na waandishi
 wa Habari kilichokuwa kikiwatangaza kuwa washindio na kujiandaa 
kuiwakilisha Nchi kwenye fainali ya mataifa ya Afrika ambapo wataungana 
na washindi wa nchi nyingine kuunda timu ya ushangiliaji ya Afrika 
United Team.
Castle
 lager wadhami wa mchezo wa mpira Afirika wametambulisha Superfans 
wawili ambao watawakilisha Tanzania katika fainali za kombe la Afica 
litakalofanyikia Afrika kusini mwanzoni wa 2013.
Akizungumza
 na waandishi wa habari jijini dar Es Salaam Meneja wa castle Lager 
Kabula Nshimbo aliwataja washindi hao kuwa ni Yahaya Hamza na Filbert 
Nestory ambao wamejipatia nafasi ya moja kwa moja kwenda nchini Afrika 
kusini kushiriki katika kuunda timu ya Ushangiliaji itakayojulikana kwa 
jina la Castle Lager United team 
Miezi
 kadhaa iliyopita superfans wetu walishiliki kwenye ushindani wa kijamii
 kupitia vyombo vya habari ili kubaini Superfans wanane kutoka nchi nne 
za Kiafirika,ambazo ni Tanzania,Zimbabwe,Zambia na Swaziland kwa ajili 
ya safari ya kipekee iliyolipiwa kwenda kuangalia kombe hilo la 
kiafirika.
Baada
 ya mzunguko wa kwanza wa shindano hilo kukamilika Tanzania, Superfans 
hao walipunguzwa na kubakia wachache ambapo watu mbalimbali nchini 
walichangua Superfans bora waliojitoa kwa ajili ya timu zao na kuvaa 
vizuri. Uchaguzi huu ulifanyika kupitia vyombo mbalimbali vya kijamii na
 mwishoni Firbert na Yahaya walitambulishwa kuwa washindi.
“Tunavyojiandaa
 kwa ajili ya mashindano ya kombe la Afrika 2013 yatakayofanyika Arika 
kusini tunataka kutengeneza mazingira ya furaha na shangwe kuhusu 
shindano  hilo,na pia kufanya mashabiki wote wa Afrika 
kushabikia timu zao na ndio maana tumefanya kampeni ya Superfans hao 
ambao wanashinda safari na tiketi ya kwenda kwenye fainali za kombe la 
Afrika,” alisema Bi Mshimo.
 Alisema,
 “mashabiki wanaendelea kuwa na umuhimu sana kwenye mashindano kama haya
 ya mpira na nivizuri kuwapongeza na kuwapa nafasi kama hii ya kipekee 
inayotokea mara moja kwenye maisha ya mtu.”
Washindi
 wote wawili watapata nafasi ya kumuangalia mcheza mpira wanaye mpenda 
moja kwa moja kiwanjani nchini Afrika Kusini. Katika washindi hawa 
wawili, Filbert ni mshabiki mkubwa wa Didier Drogba  wakati mwenzake Yahaya anampenda sana Yaya Toure.
Kwa
 ajili ya safari yao ya kwenda Afika kusini,Watanzania hao wawili 
watapumzika siku mbili katika hoteli ya Push iliyopo Johannesburg.p  Pia
 mashabiki hao, watatalii sehemu kadhaa ya mji wa Johannesburg na mwisho
 kabisa wata udhuria fainali za kombe la Afika 2013 kama wageni maalum 
wa Castle lager.
No comments :
Post a Comment