Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, December 22, 2012

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA HUDUMA YA BIMA YA AFYA KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI.



Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, (WAMA), Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa huduma za Bima ya Afya kwa vikundi vya SACCOS vya UVIMA (Umoja wa vikundi vya WAMA Tawi la Majohe lililoko wilayani Ilala) na Salma Kikwete SACCOS kilichoko Mkuranga. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Afya Mheshimiwa Dr. Hussein Mwinyi (wa kwanza kushoto). Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya Mheshimiwa Deogratias Ntukamazina (katikati) na kulia ni Afisa wa WAMA ndugu Tabu Likoko akifuatiwa na Grace Michael, Afisa Habari wa Bima ya Afya.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete na viongozi wengine wakiangalia moja ya kadi ya mwanachama wa bima ya Afya mara tu baada ya kuzindua rasmi huduma ya bima hiyo kwa wajasiriamali wa UVIMA na Salma Kikwete SACCOS kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012. Wengine katika picha kutoka kushoto kwenda kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mheshimiwa Dr. Husein Mwinyi, Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mheshimiwa Deogratias Ntukamazina na Mkurugenzi wa Mfuko huo Ndugu Emmanuel Humba.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akikabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko wa Bima ya Afya kwa Bibi Tatu Ngao, Mwenyekiti wa UVIMA mara tu baada ya kuzindua rasmi mpango huo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
Waziri wa Afya Mheshimiwa Dr. Hussein Mwinyi akimpatia tuzo ya Shujaa wa mfuko wa Bima ya Afya kwa mwaka 2012 Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa WAMA kwa jitihada zake kubwa za kumkomboa mwanamke kiuchumi na kijamii na pia katika kupigania afya kwa wote na hasa makundi maalum katika jamii. Tuzo hiyo ilitolewa baada ya uzinduzi wa huduma ya Bima ya Afya kwa vikundi vya wajasiriamali wa UVIMA na Salma Kikwete SACCOS uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo.

No comments :

Post a Comment